Home Biashara WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA: SERIKALI IKO PAMOJA NA WAWEKEZAJI, CRDB WASHIRIKI WAKUBWA...

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA: SERIKALI IKO PAMOJA NA WAWEKEZAJI, CRDB WASHIRIKI WAKUBWA WA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO NCHINI

0

Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela kutambua mchango wa benki hiyo katika sekta ya viwanda kwa kudhamini Tuzo za Rais kwa wazalishaji bora viwandani zilizofanyika jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye viwanda nchini (CTI) Bw. Subash Patel na katikati ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Innocent Bashungwa.

Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika jana kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo namna benki ya (CRDB) inavyoinua sekta ya viwanda na miradi ya maendeleo nchini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya (CRDB) Bw. Ally Laay akizungumza mambo kadhaa katika hafla hiyo.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Innocent Bashungwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa ili kuhutubia katika hafla hiyo.

Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa na wadhamini mbalimbali waliodhamini tuzo hizo.

………………………………………………………………….

 Waziri MKuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano iko pamoja na wawekezaji na wafanyabiashara, inajua changamoto wanazopitia na tayari nyingine zimetatuliwa na zinaendelea kutatuliwa.

Majaliwa alisema hayo jana Oktoba 17 wakati wa hafla ya tuzo za Rais kwa mzalishaji bora wa mwaka 2018 ambazo kampuni ya Hanspaul waliibua washindi wa jumla.

Majaliwa aliwapongezwa wawekezaji wote waliochagua kuwekeza Tanzania huku akisema uwekezaji wao katika sekta ya uzalishaji umetoa ajira zaidi 400,000.

“Rais amenituma kuwaeleza kuwa Serikali iko pamoja na nyie na anajua changamoto zinazowakabili ndiyo maana akaanzisha Wizara ya uwekezaji ili kushughulikia changamoto zenu,” alisema.

Alisema Miradi mikubwa inayoendelea hivi sasa hapa nchini ni matokeo ya faida za uwekezaji uliofanyika hapa nchini hivyo alihimiza ulipaji wa kodi.

Aidha alisema katika bajeti ya mwaka 2019/20 Serikali imefuta ada 54 ambazo zilikuwa ni kero na kikwazo katika uwekezaji hapa nchini lengo la kufanya hivyo ni kuboresha ustawi wa viwanda.

“Tunakaribisha mapendekezo yenu na msisite kutuambia pale mnapokwaza ili tuchukue hatua mara moja, tunataka muwe na imani na uwekezaji wenu hapa nchini,” alisema.

Alisema jambo la kujivunia ni hali ya usalama katika nchini hivyo mwekezaji anaweza kutabiri kesho yake na kesho ya uwekezaji wake.

Ameipongeza benki ya CRDB kwa kuwa mdhamini Mkuu wa tuzo hizo kwani udhamini wao unaongeza chachu ya ushindani wa wenye viwanda hivyo kuongeza kasi ya ukuaji na uzalishaji wa  bidhaa bora zaidi

Benki ya CRDB imeshiriki katika  Mradi wa umeme wa Stiglers Gorge, SGR  Terminal III  na upanuzi wa bandari ambapo miradi hii ikikamilika itapunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa hapa nchini hivyo kutakuwa na ustawi,”

Mkurugenzi Mtendaji wa CTI Leodegar Tenga alisema wanachama wote wa CTI wanaunga mkono mpango huo wa Serikali wa kuwa na uchumi wa viwanda.

“Hali ya kuwa na viwanda vingi na vya kutosha itaongeza ushindani katika soko la ndani na nje,” alisema.

Mwenyekiti wa CTI Subhash Patel alisema uboreshaji wa miundombinu unaoendelea utapunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa.