Home Mchanganyiko SHIRIKA LA INADES FORMATION TANZANIA LIMEITAKA JAMII KUTAMBUA HAKI NA SHERIA ZA...

SHIRIKA LA INADES FORMATION TANZANIA LIMEITAKA JAMII KUTAMBUA HAKI NA SHERIA ZA MNYAMA PUNDA

0

Mnyama aina ya Punda ambaye anapiganiwa kupata haki na sheria zake na Shirika la Inades Formation Tanzania (IFTz)

 
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Shirika la Inades Formation Tanzania (IFTz)
limeitaka jamii kutambua haki na sheria za mnyama punda pamoja na kutambua
mchango wa punda katika maisha ya jamii.
Akizungumza na vyombo vya habari  mratibu wa kuboresha maisha kupitia ustawi wa
mnyama kazi punda Fadhili  Nyingi  ambapo amesema kuwa lengo la mradi huo ni
kuboresha maisha ya watu waishio vijijini kupitia mnyama punda pamoja na  kurasimisha sekta ya punda katika halmashauri
ya wilaya ya iringa.
Lengo la kwa la mradi ni kuongeza uelewa wa watu juu ya haki
za wanyama na ufugaji bora wa Punda,mwisho wa siku watu wanatakiwa kujua punda
anatakiwa kula nini,analala wapi na anahaki gani za msingi kutoka kwa binadamu”
alisema Nyingi
Nyingi alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaongeza
uelewa kwa wananchi juu ya mnyama punda na kuwa sekta rasmi kama zilivyo sekta
nyingine.
Aidha ameeleza mafanikio waliyopata kutokana na mradi huo ikiwa
ni pamoja na kubadili mitizamo ya wananchi na kupunguzwa ukatili dhidi ya
mnyama punda.
“Mafanikio yapo toka tumeanza mradi huu,maana wananchi wengi
waliopo vijijini wameanza kubadilika kimtadhamo juu ya mnyama punda ndio maana
sasa wameanza kuacha kuuza punda” alisema Nyingi
Kwa upande wake afisa mfawidhi nyanda za juu kusini bwana Nong’ona
Solomoni amebainisha baadhi ya magonjwa yanayokumkumba mnyama punda ni pamoja
na pepo punda,homa ya farasi na vidonda.
Hata hivyo kupitia mradi huo wa Inades Formation Tanzania wamefanikiwa
kuunda vikundi 6 vya kukopeshana pamoja kutoa elimu juu ya haki za wanyama.