Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akiongea na Watalii pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Utalii waliohudhulia Uzinduzi wa Onesho la Kimataifa la Swahili la Utalii (SITE) lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Makampuni wakipokea tuzo zao katika Uzinduzi wa Onesho la Kimataifa la Swahili la Utalii (SITE) lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akiongea na Mmoja wa wadau hapa nchini katika sekta ya Utalii baada ya kuembelea mabanda katika Uzinduzi wa Onesho la Kimataifa la Swahili la Utalii (SITE) lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Khamis Kigwangala akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari katika Uzinduzi wa Onesho la Kimataifa la Swahili la Utalii (SITE) lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
**********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi amewataka watalii walioudhulia uzinduzi wa Onesho la Kimataifa la Swahili la Utalii kuweza kuwa mabalozi wazuri kwa mambo watakayoyaona hapa nchini hasa vivutio vilivyopo na kuondokana na vitisho kutoka kwa baadhi ya watu ambao wanaichafua nchi kwa madhumuni yao binafsi.
Akizungumza katika Uzinduzi huo amesema kuwa nchi hii imekuwa na vivutio vingi vya asili na vya kipekee hivyo amewataka watalii watakaporudi katika nchi zao basi wawe mabalozi wazuri.
“Wanapokuja hawa ndugu zetu kutoka nje ya nchi wanapoona wanayoyaona hapa kwa kila mtu tumepata barozi mmoja wa kwenda kutangaza nchi yetu nje ya nchi na utalii wetu kwahiyo tuhakikishe wanapata ushirikiano wa kutosha kwa yale tunayodhani yanaweza kuwasaidia kutekeleza jukumu lao la kuwa mabalozi wetu watakapofika huko kwao”.Amesema Balozi Kijazi.
Aidha Balozi Kijazi amesema kuwa Serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba wageni wote waliokuja hapa nchini kwaajili ya kushiriki tukio hilo muhimu wanaishi kwa usalama,amani na utulivu kwa muda wote watakaokuwepo hapa nchini.
Pamoja na hayo Balozi Kijazi ameongeza kuwa kasi ya kukua kwa sekta ya utalii nchini ni mzuri kwani takwimu za mwaka jana zinaeleza kuwa utalii kwa nchi zote duniani ulikua kwa wastani wa asilimia 6 kwa upande wa Tanzania utalii ulikuwa kwa asilimia 13.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Khamis Kigwangala amesema kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya kipekee hivyo ndania ya wizara yake atahakikisha Utalii unakua.
Hivyo Dkt.Kigwangala amesema kuwa Mlima Kilimanjaro umekuwa kivutio kwa watalii wengi kwasasa hivyo inatupasa tujivunio kwa hilo kwani ndania ya miaka kumi kupitia mlima Kilimanjaro tumeweza kubeba tuzo saba.