************************
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wametembelea mpaka
wa Tanzania na Msumbiji kwa lengo la kuhakikisha mpaka huo na
wananchi wa maeneo hayo wako salama, hatua hiyo imekuja
baada ya kusemekana nchini Msumbiji kunavitendo
vinavyoashilia Ugaidi vinaendelea nchini humo hayo yamesemwa
na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini CDF, General Venance
Salvatory Mabeyo, huku akisisitiza kuwa kwa sasa mpaka uko
salama na wakazi wa maeneo hayo wanatakiwa kuendelea na
majukum yao ya kila siku.
Aidha kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon
Sirro amesema hali ya nchi kwa sasa ni salama na amewataka
wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili
kuendelea kudumisha amani na usalama nchini.