NJOMBE
Naibu waziri wa maji Juma Aweso amemfuta kazi mkandarasi wa kampuni ya Eker.co.ltd aliekuwa akitekeleza mradi wa maji wa Lifua-Manda wilayani Ludewa mkoani Njombe wenye thamani ya zaidi ya mil 585 wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa madai ya kuto ridhishwa na uwezo wake.
Kampuni hiyo ilingia mkataba wa maboresho ya mfumo wa mabomba 2017 na kutakiwa kukabidhiwa serikalini 2018 jambo ambalo limeshindwa kutekelezeka hadi sasa na kusababisha kilio kikubwa kwa wananchi ambao wanai tangu huduma ya maji ikosekane kijijini kwao 2009 maradhi ya tumbo hayaishi.
Akizngumza mara baada ya kusikiliza kilio cha muda mrefu cha wakazi wa kijiji cha Lihagule ambacho ni miongoni mwa vijiji vinne vilivyokuwa vikinufaika na mradi huo kabla miundombinu yake kuchoka na kuilazimu serikali kuona umuhimu wa maboresho ,naibu waziri wa maji Juma Aweso anasema serikali imejiridhisha kuwa mkandarasi huyo hana uwezo kwa kuwa kazi iliyokuwa ikamilike baada ya miezi minne ameshindwa kuifanya katika kipindi cha miaka minne na kuagiza halmashauri kutekeleza kupitia mafundi wa ndani.
Baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo akiwemo Rejina Matei,Atu Mtweve na Laurent Muhagama wanasema kukosekana kwa huduma ya maji ya bomba kijiji kwao kumesababisha akina mama kuliwa na mamba kutokana na kufata maji katika mto ruhuu huku wengine wakidai ndoa nyingi zimevunjika kwasababu ya kutumia muda mwingi kufata maji mabondeni.
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya ludewa Adrea tsere anatumia fursa ya mkutano huo wa naibu waziri wa maji kutoa onyo kwa mwananchi ambaye hatajiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ambapo amesema yeyote ambaye hatafanya hivyo anawekwa rock up huku akiwataka wenyeviti wa vijiji kumpa taarifa ya waliosusia.