Bi.Beatrice Mwakyembe akimuhudumia mteja alietembelea banda la kampuni ya Ulinzi ya G4S katika Onesho la Kimataifa la Kiswahili la Utalii lililofanyika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Moja ya mashine ya kuhifadhi fedha (Deposita Machine) ya kampuni ya Ulinzi ya G4S ambayo ni bora kwa ulinzi wa fedha hasa katika kuhifadhi.
Mashine ya Ulinzi ya Electric Fence Security ya kampuni ya Ulinzi ya G4S ikiwa kama alama kuonesha ni namna gani inafanya kazi.
******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Kampuni ya Ulinzi ya G4S imewaletea wateja wao mashine ya kuhifadhi pesa (Diposita Machine) ambayo ni salama kwa ulinzi wa fedha za wateja wao.
Akizungumza katika Onesho la Kimataifa la Kiswahili la Utalii lililofanyika Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Masoko wa kampuni hiyo, Bi.Beatrice Mwakyembe amesema kuwa mashine hiyo itaweza kumsaidia mteja wake hasa katika kampuni au dukani kuhifadhi fedha zake kwa usalama ili kuepukana na upotevu wa fedha zake.
“Kama una duka la biashara, mashine ya deposta inaweza kukusaidia kuhifadhi pesa yako kwa usalama wa hali ya juu, na ukishaweka utapata lisiti ya fedha zako ulizoweka na kukuhakikishia usalama wa fedha zako”. Amesema Bi.Beatrice.
Aidha Bi.Beatrice amesema kuwa nje ya mashine ya kuweka fedha pia kampuni hiyo inatoa huduma ya ulinzi kama askari wenye silaha na wasio na silaha (Manned guarding) pamoja na Electric Fence Security Solutions ambazo pia inaweza kukuhakikishia usalama wa mali zako katika ofisi asu nyumbani unapoishi.