Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Watoto ya Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiongea wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kikosi Kazi cha Kuwalinda Watoto Dhidi ya Unyonyaji na Udhalilishaji wa Watoto Kupitia Mitandao mapema leo Manispaa ya Morogoro.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu Bw. Christopher Mushi kutoka Idara ya Watoto ya Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii akitoa mada wakati wa Kikao cha Kikosi Kazi cha Kuwalinda Watoto Dhidi ya Unyonyaji na Udhalilishaji wa Watoto Kupitia Mitandao mapema leo Manispaa ya Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa Kikao cha Kikosi Kazi cha Kuwalinda Watoto Dhidi ya Unyonyaji na Udhalilishaji wa Watoto Kupitia Mitandao wakijadiliana jambo wakati wa kikao hicho mapema leo Manispaa ya Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa Kikao cha Kikosi Kazi cha Kuwalinda Watoto Dhidi ya Unyonyaji na Udhalilishaji wa Watoto Kupitia Mitandao wajadiliana jambo wakati wa kikao hicho mapema leo Manispaa ya Morogoro.
………………….
Na Anthony Ishengoma –Morogoro.
Watoto wengi nchini wanakabiliwa na changamoto ya ukatili wa kingono nchini kutokana na kuongezeka kwa matumizi makubwa ya mitandao ya simu za mikononi zilizoenea kutokana na mabadiliko makubwa ya sekta ya mawasiliano duniani.
Kiwango kikubwa cha matumizi ya mitandao hasa ya simu janja za kisasa yanaendeleza ugumu wa kudhibiti watoto kuathiliwa na mitandao kutokana na jamii kutokuwa na uelewa juu ya madahara yatokanayo na mitandao hiyo.
Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Watoto ya Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kikosi Kazi cha Kuwalinda Watoto Dhidi ya Unyonyaji na Udhalilishaji wa Watoto Kupitia Mitandao mapema leo Manispaa ya Morogoro.
Bw. Kitiku aliwambia wajumbe wakikao kuwa imefikia hatua mtoto anapofanya vizuri darasani mzazi anachagua zawadi ya simu ya kidigiti kuwa ndio zawadi sahihi kwa mtoto wake kumbe hajui mtoto anapokuwa na simu hiyo anaitumia kuwasiliana na dunia kupitia mitandao.
“Mzazi unakuwa na sehemu umetulia ukidhani mambo yanaendelea vizuri kumbe mtoto chumbani anatumia simu kudukua mambo hata ambayo wakati mwingine yanamletea matatizo ambayo ni vigumu kuondana nayo’’. Aliongeza Bw. Kitiku.
Aidha Mkurugenzi huyo amewambia wajumbe wa mkutano huo kuwa kwasasa hali ni mbaya kiasi kwamba watoto wanafikia hata hutua ya kujiua kutokana na matumizi mabaya ya mawasiliano ya mtandao yanayotokana na maendeleo ya teknolojia katika sekta ya mawasiliano.
Wakati huo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu Bw. Christopher Mushi wakati akiwasilisha mada ya kuhusu hali ya ukatili dhidi ya watoto Nchini amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa kwa takwimu zilipo Nchini idadi ya watoto nchini Tanzania ni zaidi ya nusu ya watanzania wote akiwataja watoto wa kiume kufikia 48% na watoto wakike kuwa ni 51%.
Bw. Mushi ameutaja ukatili wa kingono sio lazima umaanishe tendo la ndoa lakini kinachozungumziwa sana ni uwepo wa viashiria vya ukatili wa ngono kwa kundi hili kubwa ambalo sisi kama jamii hatuna budi kulilinda na kujenga mazingira mazuri kwa maisha yao ya baadae.
Naye Bi. Thelma Dhaje kutoka Shirika la CSEMA ambaye pia ni mjumbe wa Kikosi kazi hicho amesema tatizo la Ukatili wa dhidi ya Watoto mitandaoni linazidi kuongezeka uku akiwataka wazazi kuwa makini na watoto wanapokuwa wanatumia mitandao lakini pia kuacha kusambaza picha za watoto wakati wanapofanyiwa ukatili kwa lengo la kupunguza atahari za kisaikolojia.
Kikosi kazi hicho kinakutana Mjini Morogoro kuangalia upya malengo waliojiwekea lakini pia kutafakari namna bora kufanya kampeini za kupambana na ukatili wa kingono mitandaoni ikiwemo ushauri kuhusu ujumbe unaoweza kutumika kwa jamii kupambana na ukatili huo.