NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKOA wa Pwani ,umefikia asilimia 88 ya watu zaidi ya laki nne, waliojiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa serikali ya mitaa,vitongoji na vijiji huku mkoa huo ukitarajia watu 700,000 kujiandikisha kwenye daftari hilo.
Aidha wananchi wametakiwa kuhamasika kutumia muda ulioongezwa hadi octoba 17 mwaka huu kwenda kujiandikisha na ambae hatojiandikisha aaithubutu kusogelea vituo vya kupiga kura Novemba 24 mwaka huu.
Akizungumza na wakazi wa Muhoro ,Ikwiriri huko Rufiji na Kibiti ,wakati akimalizia ziara yake ya uhamasishaji wananchi kujitokeza kujiandikisha ,mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo alisema ,jamii ina mwamko wa kuridhisha kufikia asilimia 100.
Alitaja wilaya inayoongoza kimkoa kwa uandikishaji kuwa ni Kibiti,Rufiji,Mafia,Bagamoyo,Mkuranga,Kisarawe na Kibaha hasa halmashauri ya Kibaha Mjini ikiwa imeshika mkia.
“Tutumie siku tatu zilizoongezwa na serikali ,Tuamsheamshe tunakwenda kupigia kura viongozi wetu hili lisiwe la watu wachache, tuchague viongozi wetu walio bora kutatua changamoto zetu, majuto ni mjukuuu msije kujuta baada ya wachache kutumia haki yao ya msingi'”
“Tusidharau uchaguzi huu ,tusije kulaumiana ,tusishawishiwe kwa rushwa,kipindi hiki watakuja na kila vibahashishi ,hiyo ni chambo mkiingia kingi tuuu mmenaswa”:’ ,chukueni chumvi,mifugo yao lakini mwisho wa siku wachinjieni baharini”alisisitiza Ndikilo.
Ndikilo alifafanua, uchaguzi utakuwa wa huru na haki itatendeka na endapo kama kutatokea mtu kutaka kuharibu uchaguzi atakiona.
Alibainisha, Jeshi la polisi mkoani humo pamoja na serikali limejidhatiti kudhibiti ghirba yoyote itakayojitokeza .
“Kama hukutaka kutumia haki yako ya msingi kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura siku ya uchaguzi usiende kufanya fujo kabisa katika vituo vya kupiga kura ,maana hujataka kujiandikisha sasa unaenda kufanya nini katika kituo!!??alisema kwa msisitizo.
Nae mkuu wa wilaya ya Rufiji,Juma Njwayo alieleza kwamba, kulingana na takwimu Rufiji inatarajia kuandikisha watu 64,611 lakini imeandikisha 42,243 ikiwa na asilimia 65.4 .
Mkuu wa wilaya ya Kibiti, GulamHussein Kifu alisema kuwa wilaya hiyo, ipo katika asilimia 84.45.
Wakuu hao wa wilaya,waliwaomba wananchi kutumia dakika chache za muda wao kwenda kujiandikisha kutimiza haki yao ya msingi ili wachague viongozi wanaowataka.