*********************************
Na Silvia Mchuruza
Bukoba.
Kufuatia maandalizi ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne na pili mwaka huu afisa elimu sekondari wa manispaa ya Bukoba Mwl. Emmanuel Ebeneza amezungumzia zaidi maandalizi ya mtihani huo na kuwataja watahiniwa wanaotegemea kufanya mtihiani huo.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Mwl.Emmanueli amesema kuwa watahiniwa wanaotegemea kufanya mtihani huo wamegawanyika makundi matatu kundi la kwanza ni wale walio shuleni, kundi la pili ni wale wanaojitegemea na kundi la mwisho ni wale wanaorudia mtihani hili kukidhi vigezo vya kufanya mtihani wa kidato cha nne.
Aidha ameongeza kuwa jumla ya watainiwa wote kupitia makundi hayo ni 2847 ikiwa watainiwa walio shule ni 2012 ambapo wasichana ni 1237 na wavulana ni 1080 pia na wanarudia mitihani wavulana ni 217 na wasichana ni 240 pamoja na wale wanaofanya mtihani huo hili kukidhi vigezo wavulana ni 36 na wasichana 37.
Pia amesema kuwa mtihani huo wa kidato cha nne unategemea kufanyika tarehe 04/11 mpaka tarehe 22/11 mwaka huu ikiwa manispa ya bukoba itakuwa navituo 30 kwa watahiniwa walio shuleni na vituo 7 kwa wale wanaojitegemea.
Vilevile amewataja watahiniwa wanaotarajia kufanya mtihani wa kidato cha pili katika manispa ya Bukoba ni 2714 ikiwa wasichana ni 1476 na wavulana ni 1238 ambapo mtihani huo unatarajiwa kuanza tarehe 11/11 mpaka tarehe 22/11 mwaka huu.
Sambamba na hayo amewaomba wanafunzi wa manispaa ya Bukoba mkoani humo kuhakikisha wanajiandaa vyema kuelekea mitihani hiyo hili kuweza kufikia malengo yao na kuwaomba wazazi kuwasisitiza bidii katika masomo ya watoto wao.