Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(katikati) akizungumza na wakazi mbalimbali wa Manispaa ya Tabora wakati wa ukaguzi wa zoezi la orodheshaji wananchi wenye sifa na kuwahamasisha ili waweze kushiriki uchaguzi ujao.
Baadhi ya wapiga debe na abiria katika Stendi kuu ya Tabora wakimsililiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(hayupo katika picha) wakati akizungumza na wakazi mbalimbali wa Manispaa ya Tabora wakati wa ukaguzi wa zoezi la orodheshaji wananchi wenye sifa na kuwahasisha ili waweze kushiriki uchaguzi ujao.
………………….
NA TIGANYA VINCENT
WAKAZI Mkoani Tabora wametakiwa kutumia haki yao ya kidemokrasia kwenda kwenye Vituo vya uandikishaji kwa ajili ya kujiorodhesha ili wawe fursa ya kuchaguliwa na kuwachagua viongozi wa Mitaa na Vijiji wenye mtazamo wa kuwasaidia kushiriki kikamilifu katika kuwaletea maendeleo
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akizungumza na wakazi mbalimbali wa Manispaa ya Tabora wakati wa ukaguzi wa zoezi la orodheshaji wananchi wenye sifa kwa ajili ya uchaguzi ujao.
Alisema kitendo cha baadhi yao kutojiandikisha kinaweza kuwasababishia hasara kutokana na kuchaguliwa kiongozi asiye na mtazamo wa kuwaongoza vizuri katika kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Kati ambao msingi wake ni viwanda.
“Adhabu ya kutoshiriki uchaguzi ni miaka mitano…usipojiandikisha unaweza kusababu watu wakachagua kiongozi ambaye usingependa akuongoze…kwa hiyo ni vema uende ukajiorodheshe ili kura yako moja iweze kutupatia kiongozi mzuri ambaye atakwenda na kasi ya nchi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda” alisema.
Mwanri alisema ni vema kwa wananchi ambao bado hawajajiorodesha kushiriki uchaguzi ujao kutumia siku zilizobaki kwenda katika vituo kujiandikisha kwa ajili ya kupata kibali cha kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Alisema uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni muhimu kwa kuwa ndio utsaidia kuwapata viongozi ambao watakuwa karibu na wananchi siku zote na ndio watasaidia kupeleka matatizo mbalimbali katika uongozi wa juu.