Home Mchanganyiko SHILINGI BILIONI 1 NA MILIONI 216 ZAMFANYA MBUNGE JASSON RWEIKIZA KUTOA USHAIDI...

SHILINGI BILIONI 1 NA MILIONI 216 ZAMFANYA MBUNGE JASSON RWEIKIZA KUTOA USHAIDI MAHAKAMANI.

0

Na Silvia Mchuruza.
Bukoba.
Mdaiwa  katika kesi  namba 12 ya mwaka  2016  ya madai ya shilingi bilioni 1 na milioni 216 iliyofunguliwa na mbunge wa jimbo la bukoba Vijijini Jasson Rweikiza mahakama kuu  Kanda ya Bukoba dhidi ya mdaiwa Novatus Nkwama,Mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi ( CCM ) Mkoa wa Kagera ameanza kutoa ushahidi wake.

 

Novatus Nkwama ,akiongozwa  na mawakili wawili ambao ni Dastan   Mujaki na Jovin  Rutainulwa aliieleza mahakama kuu mbele ya Jaji Dk.Ntemi Kilekamajinga wa mahakama hiyo kuwa alistaafu nafasi ya uenyekiti ccm halmashauri ya Bukoba  mwaka 2017 na sasa ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM ,Mkoa wa Kagera.

 

Hata hivyo mdai wa kesi hiyo Mbunge Rweikiza amesema kuwa mdaiwa alimdhalilisha akiwa katika studio za redio karagwe ambapo mdaiwa amekana shitaka hilo na kusema kuwa toka azaliwe hakuwawi kuziona studio za redio hiyo na kuwa ajui zilipo na kumtaka mdai kuleta mashaidi   hili kutoa ushaidi juu ya dai hilo.

“Naiomba mahakama hii kupitia radio karagwe nanaomba ofisi ya redio hiyo kuleta kitabu cha wageni hili kudhibitisha kama niliwahi kuingia katika studio  za redio karagwe au kuleta sauti iliyosikika nikimkaahifu ambapo mdai anasema nilimkaahifu” alisema Novatus Nkwama

Hata hivyo Mdaiwa aliieleza mahakama kuwa zaidi ya hapo kama angethubutu kuingia katika studio hiyo na kutamka maneno hayo mdai alitakiwa kumfikisha mtangazaji na mhariri mahakamani kuthibitisha hayo lakini hakufanya hivyo.

Sambamba na hayo wakili wa mdaiwa aliendelea kumuuliza maswali mbalimbali mdaiwa juu ya kuilezea mahakama kwa usahihi kabisa juu ya ushaidi alionao.

Jaji dk.Kilekamajinga,alisema kesi hiyo ni ya waka 2016 inatakiwa kumalizika mwaka huu hivyo aliwataka upande wa utetezi kuwaanda mashahidi wao haraka.

Aliongeze mwaka huu hadi kufika tarehe 15 Desemba kesi itakuwa imekamilika na kutolewa hukumu.