Home Mchanganyiko Mikasa ya Mimba Mashuleni Bado Kikwazo Wanging’ombe

Mikasa ya Mimba Mashuleni Bado Kikwazo Wanging’ombe

0

***************************

NJOMBE

Serikali wilayani Wanging’ombe imetangaza kuanza kuwatia mbaloni viongozi wa wa vijiji ambavyo vitabainika kukaliwa na wanaume wenye mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi kwa lengo la kusuru ndoto za watoto wengi wanaoshindwa kuendelea na masomo baada ya kupata ujauzito.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Comrade Ally Kassinge kupokea ripoti kutoka idara ya elimu ikionyesha kuwa katika kipindi cha kuanzia  januari hadi octoba 2019 wanafunzi 9 wamepata mimba huku shule ya sekondari Usuka ikitajwa kuwa na mimba mbili hatua ambayo inamkasirisha na kuamua kutoa tamko.

Mwishoni mwa mwaka jana Kassinge alitangaza mikakati 20 ya kudhibiti mimba mashuleni ambapo baadhi ya mikakati hiyo ikiwa ni marufuku ya kuwatumia wanafunzi kusimamia harusi, kampeni ya ujenzi wa mabweni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi ambao maeneo yao yatabainika kuwa na wanaume wenye mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi na kuwasabishia mimba

Tamko lililotolewa na mkuu wa wilaya linaifanya Fullshangwe kuzungumza na Amani Mwakomu ambaye ni mkuu wa shule ya Usuka yenye mimba nyingi zaidi wilayani humo pamoja na mwenyekiti wa bodi Exaud Sapali ambao wanaeleza hatua ambazo wanazichukua .

Kwa upande wa wanafunzi akiwemo Helena Msigwa  wanasema endapo mabweni yangejengwa kwa kila shule tatizo hilo lingedhibitiwa kwa kuwa wanafunzi wengi wanarubuniwa mitaani na wawapo njiani kwenda na kurudi shule.