|
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani kuhusiana namna watakavyotumia mashindano ya Korogwe Mini Marathon kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa |
MKUU wa wilaya ya Korogwe kulia Kissa Gwakisa akimkabidhi namba ya ushiriki mmoja wa wananchi wa wilaya ya Korogwe Noah Gondwe ambao wamejitokeza kuajiandikisha kushiriki mashindano ya Korogwe Mini Marathoni yatakayofanyika leo Jumapili ambayo yameandaliwa na Mkuu huyo wa wilaya
|
MKUU wa wilaya ya Korogwe kulia Kissa Gwakisa akimkabidhi namba ya ushiriki mmoja wa wananchi wa wilaya ya Korogwe Magesa Kuboja ambao wamejitokeza kuajiandikisha kushiriki mashindano ya Korogwe Mini Marathoni yatakayofanyika leo Jumapili ambayo yameandaliwa na Mkuu huyo wa wilaya |
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha kushiriki kwenye mashindano ya Korogwe Mini Marathon yatakayofanyika kesho Jumapili wilayani Korogwe
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa katikati akiwa na baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kujiandikisha kushiriki kwenye mbio za Korogwe Mini Marathon ambazo zitafanyika kesho Jumapili wilayani Korogwe
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kushoto akiwasikiliza wanariadhaa ambao wamefika wilayani humo kutoka mkoani Arusha kujiandikisha kushiriki kwenye mashindano ya Korogwe Mini Marathon yatakayofanyika kesho Jumapili mjini humo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa aliyesimama katikati akiwa kwenye picha ya pamoja nao
MASHINDANO ya Riadha ya Korogwe Mini yanatarajiwa kufanyika kesho Jumapili mjini hapa huku yakitumika kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.
Mashindano hayo yameandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa
Alisema lengo kubwa ni kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni kutimiza miaka 20 ya kumuenzi lakini pia kuchangia maendeleo wilaya ya Korogwe huku akitoa wito kwa wananchi wajitokeza waungane pamoja kushiriki kwenye mashindano hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa alisema kwamba mashindano hayo watatumia muda mchache ambapo wataanza saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa mbili nusu asubuhi yatakuwa yamemalizika.
Alisema pamoja na kumuenzi baba wa Taifa ambaye alipenda demokrasi ya nchi yetu na ndio maana alipigania sana vyama vingi kwenye nchi yetu na hadi kufikia kusema wachache wapewe mpaka hivi leo kuna vyama vingi.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba mambo makubwa aliyoyafanya Mwalimu Nyerere mpaka leo yanaendelea kufanywa na Rais aliyepo madarakani Dkt John Magufuli kwa kuendelea kuenzi demokrasia ndio maana alihamasisha nchi nzima watanzania waendelee kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura kwenye uchgaguizi wa serikali za mitaa.
Alisema kwamba Rais Dkt John Magufuli alisema watu wajitokeza kwa wingi kuiandikisha kwenye daftari la kupiga kura huku akieleza kwamba watakaofika kwenye mashindano hayo watapewa hamasa ya kwenda kujiandikisha na watatoa usafiri kwa wale ambao hawajiwezi.
“Sisi kama ofisi ya DC kwa wale ambao watakuwa hawajiwezi ili tutawapeleka waende kujiandikisha Korogwe lakini pia Korogwe Mini Marathon italeta hamasa kwa wananchi kujiandikisha na kujitokeza kwa wingi kwenye kujiandikisha “Alisema
“Lakini pia niwaambie kwamba ile mvua au jua tutaendelea kuhamasisha wananchi kujiandikisha tokea tuanze tumeona mafanikio Halmashauri ya wilaya tayari juzi wamejiandikisha asilimia 42 hivyo ninaamini kwamba siku zilizobakia tutavuka lengo ambalo tumewekewa “Alisema DC Kissa.
Naye kwa upande wake mmoja wa wananchi wa Mtaa wa Mbeza wilayani Korogwe Magesa Luhoga alisema kwamba wao wamejiandaa vema kushiriki kwenye mashindano hayo na kwamba atashiriki kwenye kilimota 10.
Alisema mashindano hayo ni jambo jema kwa wananchi wa wilaya ya Korogwe huku akimpongeza Mkuu wa wilaya hiyo kwa kuandaa mashindano hayo kwani yataimarisha maendeleo huku wananchi wakiimarisha miili yao.
Hata hivyo kwa upande wake Bakari Nchimbi ambaye ni meneja mauzo kampuni ya TBL alisema kwamba watashiriki kwenye mashindano hayo ili kuunga mkono juhudi za mkuu huyo wa wilaya za kuhamasisha maendeleo
Hata hivyo naye kwa upande wake Noah Gondwe ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mnyuzi alisema kwamba watashiriki mashindano hayo kwa kuhakikisha wanamuunga mkono Mkuu huyo wa wilaya.