Home Burudani Mwimbaji Esther Kusekwa Hajakata Tamaa “Anatamani Kukutana na Rais Magufuli”

Mwimbaji Esther Kusekwa Hajakata Tamaa “Anatamani Kukutana na Rais Magufuli”

0
Mwimbaji wa nyimbo za injili na kijamii jijini Mwanza, Esther Kusekwa (katikati) amesema ana kiu na ndoto kubwa ya kukutana ana kwa ana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Kusekwa ameyasema hayo Oktoba 11, 2019 alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) kupata Baraka zake baada ya kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru Oktoba 14, 2019 mkoani Lindi.
Kwa sasa Kusekwa anatamba na Albamu mbalimbali za Injili na za kuhamasisha maendeleo ikiwemo Magufuli ni Jembe.