Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto Leo amekutana na Sheikh wa wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum ambaye pia Ni Mwenyekiti wa Kamati ya Amani kufanya nae mazungumzo Pamoja na kutoa shukrani kwa jinsi Viongozi hao wa dini wanavyoshiriki katika kuliombea Taifa na Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza na Sheikh Alhad Mstahiki Meya Omary Kumbilamoto amesema Kamati ya amani imekuwa na mchango mkubwa katika kulifanya jiji la Dar es Salaam kutulia na mabishano ya dini kumalizika kabisa.
Kumbilamoto pia alitumia nafasi kumweleza Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Amani juu miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Manispaa ya Ilala .
“Mh Rais Dk John Pombe Magufuli ametupa bilioni 12.5 kwa ajili ya ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti, Bilioni 13.5 kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la kisutu na tayari fedha zote hizi zipo hazina tayari kwa ajili ya kutekeleza miradi hii miwili mikubwa ya kimkakati” ameeeleza Mstahiki Meya Omary Kumbilamoto.
Kumbilamoto Moto pia amemweleza Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam kuwa Mh Rais Dk John Pombe Magufuli ametoa Bilioni 1.5 kwa ajili ya Hospitali ya Kivule ambayo itakuwa Hospitali ya wilaya ya Ilala ambayo ipo katika hatua za mwisho za ujenzi.
Mstahiki Meya Kumbilamoto ameeleza kuwa pia jumla ya Shilingi Milioni 500 zilitolewa kwa ajili ya upanuzi wa Hospitali ya kwa Mnyamani na tayari ujenzi umekamilika .
Mstahiki Meya Omary Kumbilamoto alitumia wasaa huo kutoa mwaliko kwa Kamati ya Amani kutembelea miradi yote iliyofadhiliwa na Mh Rais Dk John Pombe Magufuli hili waweze kujionea kazi iliyofanyika katika Manispaa hiyo chini ya serikali ya awamu ya tano.