Mkurugenzi wa Taasisi ya Promised Eden Environmental Care (PEEC) iliyopo Karagwe, Kagera, Tanzania, East Africa, Ascarlyon Lufurano akionesha mapapai yanayolimwa na Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Pili ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa 2019 Mkoa wa Singida.
Ascarlyon Lufurano akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao katika maonyesho hayo.
Ascarlyon Lufurano akiwa na Mratibu wa Miradi wa Taasisi hiyo, Leonard Bandio.
Mhandisi Mohamed Kimia wa Shirika la Sema (kushoto) akielekeza namna ya kutumia pampu ya maji ya kamba jinsi inavyofanya kazi.
Mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Sabasaba chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Mkoa wa Singida, Janifa Olais (kushoto) akimuonesha Gelard Kilomo mfuko wa kitambaa ulioshonwa na
chuo hicho.
Wanafunzi wa chuo hicho wakiwa kwenye banda lao na walimu wao.Katikati waliosimama ni mkuu wa chuo hicho, Fatuma Malenga na kushoto ni Mwalimu, Maria Joram.
Mwanafunzi wa fani ya umeme wa majumbani wa chuo hicho, Stephen Lucas (katikati) akimuekeza namna ya kuwasha taa, Ester Mvati alipotembelea banda hilo. Kulia ni Mwanafunzi, Omari Salum.
Mjasiriamali wa kuuza dawa za asili kutoka Aspera 4 Women, Sophia David (kulia) akitoa maelezo ya matumizi ya dawa kwa wananchi waliotembelea banda lake.
Muonekano wa banda la wajasiriamali wa dawa za asili zitokanazo na mimea.
Muonekano wa mabanda ya maonyesho hayo.
Mzee Hassan Magomba kutoka Urambo Tabora akiwaelekeza wanafunzi wa Veta namna mashine ya kuangulia vifaranga vya kuku inavyofanya kazi.
Soud Bakari (wa pili kushoto) akiwaelekeza wanafunzi wa Veta jinsi mashine ya kuangulia vifaranga vya kuku inavyofanya kazi.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Poly Machinery Com.LTD, Amos Leng’oko (katikati) akiwaelekeza wananchi waliotembelea banda lao jinsi ya mashine ya kusaga mahindi inavyofanya kazi.
Meneja Masoko wa Deve General Supplies Company, Gisela Denis akiwaelekeza wakina mama waliotembelea banda la kampuni hiyo jinsi ya kutumia vitanda vya kujifungulia na kulalia wagonjwa.
Gisela Denis akielekeza namna ya kutumia kitanda cha kujifungulia.
Mtaalamu wa kutengeneza majiko ya kisasa ambayo yanatumia mkaa na kuni kidogo na kutunza joto, Omari Komba (wa pili kulia) akitoa maelezo jinsi ya kutumia majiko hayo.
Mjasiriamali wa kutengeneza vyungu kutoka Kondoa Dodoma, Sophia Mumba (kushoto) akielekeza jinsi ya kutengeneza bidhaa hizo.
Mjasiriamali wa kusindika vyakula vya kimiminika kama pilipili, jamu ya asali, karanga na vinginevyo kutoka Madima Enterprises ya Manyara, Lilian Joseph (kulia) akielezea ubora wa
bidhaa zake.
Mjasiriamali Hyasinta Wanchelele (kulia) kutoka Mwanza, akimuonesha dagaa Fanuel Dissa wanao tengenezwa na kampuni yake.
Wajasiriamali Anna John na Boniface John kutoka Chonde Group mkoani Manyara wakiwa mbele ya bidhaa zao.
Mjasiriamali kutoka Kamshuu Food Industry, Shufaa Mubago Arusha akiwa na bidhaa zake katika maonesho hayo.
Mjasiriamali Esther Songoi kutoka Wisdom Food Products jijini Mwanza akiwa na bidhaa zake.
Mjariamali Theresia Mbili kutoka 2 Super Unga wa Ubuyu mkoani Mara akiwa mbele ya bidhaa zake.
Mjasiriamali wa kutengeneza Mvinyo kutoka Kampuni ya Epac Products Centre ya Jijini Dodoma akiwa mbele ya bidhaa zake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Panako Products ya Nansio Ukerewe inayotengeneza Mvinyo Rosela, Paschal Mahotola (kushoto) akizungumza na wananchi waliotembelea banda lake katika maonesho hayo.
Mjasiriamali Pasikazia Sebastian (kushoto) kutoka Kagera Organic Farmers Community (Kaofaco Food Processing) akiwaelezea wananchi ubora wa bidhaa wanazo zitengeneza.
Wajasiriamali Soud Rajab (kulia) na Daniel Crown kutoka Misuna Oil Mill wakiwa mbele ya bidhaa zao kwenye maonesho hayo.
Afisa wa Kampuni ya Faida Mali, Lazaro Mnkumbu (katikati) akitoa maelekezo jinsi ya kutumia mashine ya kupandia mbegu zinazosambazwa na kampuni hiyo.
Watoto wakipata burudani ya kubembea katika maonesho hayo. Bembea hiyo imetengenezwa na Mjasiriamali Kapalata wa mjini Singida.
Mjasiriamali ambaye ni mwandishi wa vitabu Mwalimu Jilu Muna Mpanda wa mkoani Singida, akionesha kitabu alichokiandika cha Chimbuko la koo mbalimbali za Arimi (Wanyaturu $ Wanyiramba)