Home Michezo MAN CITY WAPOTEANA NYUMBANI,CHELSEA YANG’ARA LIGI KUU ENGLAND

MAN CITY WAPOTEANA NYUMBANI,CHELSEA YANG’ARA LIGI KUU ENGLAND

0

Winga wa kimataifa wa Hispania mwenye asili ya Mali, Adama Traore akishangilia baada ya kuifungia mabao yote mawili Wolverhampton Wanderers dakika za 80 na 90 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad leo PICHA ZAIDI SOMA  HAPA

Michy Batshuayi akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la nne dakika ya 89 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Southampton leo Uwanja wa St. Mary’s, Hampshire. Mabao mengine ya Chelsea yamefungwa na Tammy Abraham dakika ya 24, Mason Mount dakika ya 17 na N’Golo Kanté 40, wakati la Southampton limefungwa na Danny Ings dakika ya 30 PICHA ZAIDI SOMA  HAPA