Na Joyce Kasiki
“Ni muhimu kwa mtoto wa darasa la awali kuanza kujifunza kwa kutumia zana au vifaa na michezo mbalimbali kabla ya kuanza kujifunza kwa Kuandika na penseli kwenye daftari kwa sababu uwezo wa ubongo wake kwa kipindi hicho ni kuona kutambua.”
Hayo ni maneno ya mratibu wa wanafunzi wa darasa la awali katika shule ya msingi ya mchepuo wa kingereza ya Capital iliyopo jijini Dodoma Issa Idrisa wakati mahojiano maalum kuhusu ujifunzaji na ufundishaji wa wanafunzi wa darasa la awali ambao umri wao mara nyingi ni kuanzia miaka mitatu hadi mitano.
Anasema,katika kipindi hicho ,ubongo wa mtoto unakuwa hajakomaa kusikiliza na kushika mambo mengi tofauti na watoto wa madarasa ya juu.
Mwa limu huyo anasema,mbalimbali na kutumia vifaa na michezo mbalimbali baadaye wanafunzi hao huanza Kuandika kwa kijiti ardhini na wanapoanza kuelewa ndipo huanza kuandika kwa penseli.
“Kwa mfano hapa shuleni kwetu,watoto wenye umri wa miaka mitatu ,minne na mitano wanafundishwa kwa kutumia zana za kushika na kwa kuona ,lengo kubwa ni kumsaidia mtoto kuelewa haraka na kukumbuka .” Anasema na kuongeza
“Pia katika kundi hilo wanafundishwa kwa kuwagawa kulingana na umri na uwezo wa kila mtoto,maana huwezi kuwachanganya wote katika darasa moja kwani wana umri na uelewa tofauti.”
Anasema katika darasa hilo la awali wale wenye umri wanaofikisha umri wa miaka mitano wanaoanza Kuandika kwa kutumia penseli kwani wanakuwa tayari wameshapitia kipindi cha malezi cha kujifunza kwa kuchelewa vitu na kuona na wakati huo sasa wanakuwa wanaandaliwa kwa ajili kwenda darasa la kwanza.
“Hapa kwetu wanafunzi wanafundishwa kwa kutumia projector,toys,mipira,Kamba,bembea,kukimbia na michezo mingine mingi,hii inampa mtoto uchangamshi,kuelewa na kutenda shule kulingana na umri wake.”
Kwa upande wake mwa limu Mkuu wa shule hiyo Muhammad Mukhsein anasema,ufundishaji wa darasa la awali unatoka mwa limu kuwa makini ili kila mtoto aelewe kile anachofundishwa na kukishika taratibu kulingana na umri wake na uwezo wa ubongo wake wa kushika mambo.
Anasema,na ili mtoto aelewe kwa urahisi zaidi,mwalimu anapaswa kupita meza hadi meza ili kumsaidia mtoto mmoja mmoja ambapo kwa wale wenye umri wa miaka mitatu wanapaswa kutumia nyimbo na michezo zaidi kwani umri huo ni wa kulelewa na kukua huku wakijifunza taratibu.
Anasema darasa la kundi hilo halipaswi kuwa na wanafunzi wengi ili mwalimu aweze kufundisha kwa urahisi na wanafunzi waweze kumwelewa kwa haraka zaidi bila mtoto atapewa vitu vitu was tofauti na umri wake na kumpa shida katika uelewa.
Mwalimu Mukhsein anasema,pia mtoto anapaswa apate muda wa kupumzika,kucheza na kufanya shughuli za kutengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia zana ili kukuza ufahamu wa ubongo wake.
“Wanafunzi wa darasa la awali (baby class) hapa kwetu ,saa Sita kamili wanamaliza vipindi,wanakula chakula cha mchana kisha wanaenda kulala ili kupumzisha ubongo,na saa tisa alasiri wanaamshwa ,wanaangalia tv vipindi vya watoto au wanaenda kucheza kwa ajili ya kuwachangamsha na kisha wanaoanza Safari ya kurudi nyumbani, “anasema mwalimu Mukhsein
Kwa upande wake mwalimu Mkuu Msaidizi shuleni hapo Idd Kibwana anasema,watoto wa madarasa ya awali wanatakiwa kutengenezewa mazingira rafiki ya ufundishaji na kujifunza ili wapende shule ikiwemo michezo mbalimbali na vitu vya kuchezea.
Anasema watoto hao wanapaswa kujifunza kwa kuona na kutenda wenyewe kwa kuwawekewa vitu kwa ajili ya utambulisho wa vitu na matendo mbalimbali hapo wanafurahi lakini pia huwafanya kupenda shule.
“Shule zitengeneze mazingira ya mtoto kupenda shule na kujifunza mazingira mabaya hufanyika mtoto achukie shule tu ikifanya hivyo watoto wa madarasa ya awali watapenda kujifunza .”Anasema mwalimu huyo