Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akizungumza wakati wa Bonanza la
Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Serikali na wananchi wa jiji la
Dodoma wakifanya mazeozi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo
lililoandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.
Timu za Mpira wa miguu za Serikali na Baobao Queens ya Jijini
Dodoma zikichuana vikali katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lililofanyika leo katika
Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma ambapo timu ya Serikali ilishinda kwa
magoli matatu dhidi ya goli moja.
4.Timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo ikiwa uwanjani ikishindana na timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi ambapo timu hiyo iliibuka kidedea katika Bonanza la Michezo
lililoandaliwa na Wizara hiyo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri
Jijini Dodoma.
********************************
Na Mwandishi wetu – WHUSM
05/10/2019,Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo amesema kuwa
Bonanza la Michezo litaendelea kufanyika kila baada ya miezi miwili na
litahusisha michezo mbalimbali.
Bw.Singo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipozungumza wakati
akishukuru Watumishi wa Serikali na wananchi wa Jijini la Dodoma
waliojitokeza kushiriki Bonanza hilo.
“Bonanza hili litafanyika kila baada ya miezi miwili lengo ikiwa ni
kuimarisha afya zetu pamoja na kuimarisha upendo,amani na mshikamano
tulionao Tanzania”alisema Bw.Singo.
Aidha Bw.Singo amesema kuwa Bonanza hilo litashirikisha michezo
mbalimbali ikiwemo mbio za taratibu,mazoezi ya viungo, mpira wa
miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na michezo mingine.
Naye Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Bw.Daudi Manongi amesema
kuwa Bonanza hilo limekuwa na faida nyingi kwani limewakutunisha
Watumishi wa Serikali na Wananchi wa Jiji la Dodoma katika kuimarisha
afya zao na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza kazi zao.
Katika bonanza hilo timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya habari,Elimu na
timu ya Joggin kutoka Dodoma ziliibuka washindi ,huku timu ya mpira wa
miguu ya Serikali ikiifunga magoli matatu timu ya Boabao Queens ya Jiji
la Dodoma iliyoambulia goli moja.