Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Tawi la Taasisi ya Sachia Society katika ,Mtaa wa Sekondari kata ya Makutopora mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa utawala wa Sachia Society Bi.Nsia Paul ,akitoa hotuba wakati wa Uzinduzi wa Tawi wa Taasisi hiyo katika ,Mtaa wa Sekondari kata ya Makutopora mjini Dodoma.
Katibu wa Sachia Society Debora Dercos akiongea wakati wa uzinduzi wa Tawi la Taasisi hiyo ya katika ,Mtaa wa Sekondari kata ya Makutopora mjini Dodoma.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Dodoma Bw.Fidelis Shauritanga,akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Tawi la Taasisi ya Sachia Society katika ,Mtaa wa Sekondari kata ya Makutopora mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde,akikata utepe wakati wa Uzinduzi wa Tawi la Taasisi ya Sachia Society katika ,Mtaa wa Sekondari kata ya Makutopora mjini Dodoma (katikati) ni Mkurugenzi wa utawala wa taasisi hiyo Bi.Nsia Paul upande wa kushoto ni Katibu wa Sachia Society Debora Dercos
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde,akigawa kadi za bima ya afya (NHIF) Kwa watoto 100 ambazo zimetolewa na taasisi ya Sachia Society kwa watoto wanaoishi katika kaya maskini jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde,akiimba wimbo na watoto wanaoishi katika kaya maskini ambao wamepewa kadi za bima ya afya (NHIF) kutoka kwa Taasisi ya Sachia Society jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi katika kaya maskini ambao wamepewa kadi za bima ya afya (NHIF) kutoka kwa Taasisi ya Sachia Society jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
…………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Taasisi ya Sachia Society inatarajia kuwapatia watoto 100 kadi za bima ya afya (NHIF) wanaoishi katika kaya maskini jijini Dodoma ili waweze kupata huduma za afya kwa urahisi.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa utawala wa taasisi hiyo,Bi.Nsia Paul wakati akitoa kadi hizo kwa watoto 33 wa mtaa wa sekondari kata ya Makutupora, jijini Dodoma.
Mkurugenzi huyo amesema taasisi hiyo inatoa huduma bure kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 7 hadi 17 ambao ni yatima, wenye ulemavu, wanaoishi kaya maskini na wasichana waliokosa nafasi ya kujiendeleza kielimu.
Amesema watoto 100 watapatiwa kadi hizo kwa awamu ya kwanza katika mitaa nane ya jiji hilo.
“Wazo hili ni la Mkurugenzi wetu mkuu Herieth Paul ambaye alilipata alipokuwa akimalizia masomo yake ya elimu ya sekondari nchini Canada akiwa na umri wa miaka 17, aliona kufanya jambo la ziada kwa kuwasaidia watoto wenye umri mdogo,”amesema.
Paul amesema lengo la taasisi hiyo ni kuhakikisha kwamba baadhi ya watoto wanapata nafasi ya kutimiza malengo yao waliyokusudia.
Ametoa wito kwa asasi nyingine za kiraia kujielekeza katika kusaidia watoto na vijana walio katika mazingira magumu ili waweze kutimiza ndoto zao na kushiriki kwenye harakati za kimaendeleo.
Kadhalika, amesema taasisi hiyo inatarajia kujenga kituo chake Dodoma ambacho kitakuwa na miundombinu mbalimbali.
Akikabidhi kadi hizo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde amewataka wananchi kujiunga na bima ya afya kwa kuwa zinasaidia kurahisisha kupata matibabu pindi wanapokubwa na maradhi.
Ameshukuru taasisi hiyo kwa kuwagusa watoto hao ambao watakuwa na uhakika wa afya zao kwa mwaka huu.
Ametoa rai kwa mashirika na wadau wengine kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.