********************
Licha ya kaya 27 elfu ambayo ni sawa na asilimia 16 ya wakazi wa mkoa wa Njombe wamefanikiwa kujiandikisha katika mfumo mpya wa mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa CHF.
Kiwango hicho kinaonekana kuwa kidogo zaidi jambo ambalo linamfanya mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka kutoa agizo kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo kuifanya agenda ya wananchi kujiunga katika mfuko wa chf kuwa agenda ya kudumu huku akitaja agenda nyingine za kupewa kipaumbele kuwa Udumavu na maambukizi ya virus vya ukimwi.
Olsendeka ametoa agizo hilo wakati akizindua mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa wa CHF mkoani humo na kueleza kwamba mpango wa serikali ni kufikia asilimia 50 ya kaya kutumia mfuko huo ifikapo 2020 kwa lengo la kurahisisha utolewaji wa huduma za afya kwa wananchi kwa gharama naafuu.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu ifikapo octoba 8 hadi 14 ,zoezi ambalo litaongozwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC inayozunguka nchi nzima kwa ajili ya maboresho.
Awali akifafanua kuhusu maboresho ya mfuko huo Mawazo haule ambaye ni mratibu wa CHF mkoa wa Njombe amesema serikali imetanua wigo wa matibabu kutoka hatua ya awali ya matibabu yani zahanati hadi kufikia hospitali za rufaa kwa gharama yakutoka elfu kumi hadi kufika elfu 30.
Shekh wa msikiti wa mkoa wa Njombe Rajabu Msigwa na Sada Msangi ni baadhi ya wakazi wa mkoa huo wanasema maboresho hayo ymekuwa na tija kwa wananchi hivyo wanahamasika kujiunga na mfuko huo wa bima ya matibabu.
Kwa Mujibu wa Sensaya 2012 mkoa wa Njombe una watu takribani laki 702,075