Naibu waziri wizara ya kilimo Mhe Hussein Bashe akiongea na wanaushirika wa wilaya ya Chato hivi karbuni katika jitihada za kukufua kiwanda cha kuchakata pamba (chato Ginery) kilichopo wilayani hapo.
Naibu waziri wizara ya kilimo Mhe Hussein Bashe akikagua shehena ya pamba katika kiwanda cha KOMWE kilichopo kahama hivi karibuni lengo likiwa kujua namna ambavyo wananunua pamba ya wakulia.
Na Bashiri Salum,Wizara ya kilimo,Chato
Naibu Waziri Kilimo Mhe. Husseni Bashe leo tarehe 02.10. 2019 amesema Wizara inaandaa mpango wa kutoa zawadi kwa kila kata itakayofanya vizuri katika kilimo kwa kuongeza uzalishaji na tija.
Watendaji wa Kata na Vijiji ni moja kati ya Viongozi watakao pata zawadi binafsi kutokana na umuhimu wao katika kukisimamia kilimo pamoja na masoko ya mazao.
Akiongea wakati wa ziara yake Wilayani Chato Mhe. Naibu Waziri amesema kwamba Wizara ya Kilimo imeandaa fomu maalumu ambayo itatumika katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za wakulima zoezi ambalo litarahisiha ufuatiliaji wa shuhuli za kilimo.
Mhe. Bashe amesisitiza kwamba fomu hiyo itakayokuwa na taarifa za wakulima zitasaidia kuendeleza kilimo kwa kuwa itaongeza usamamizi kwa viongozi wa kijiji wataalamu wa kilimo na ngazi za watoa maamuzi.
“Kama wizara tutashirikiana na maafisa kilimo ngazi ya wilaya kuhakikisha kata itakayofanya vizuri itapewa zawadi ambayo bado kwa ajili ya kata hiyo na zawadi kwa viongozi wote wa kijiji”. Alisema Bashe.
Fomu hizo zimeandaliwa kupata taarifa kuhusu kwanini mkulima mwaka uliopita alifanikiwa au hakufanikiwa,alitumia pembejeo zipi za kilimo kwa mwaka uliopita ambapo maboresho yataanzia hapo alifafanua Mhe.Bashe.
Aidha katika utekelezaji wake kamati maalumu zitaundwa katika ngazi ya Halmashauri ambazo zitaandaa vigezo vya kuipata kata iliyofanya vizuri wakati wizara ikiandaa aina ya zawadi kulingana na aina ya mazao katika kata husika.
Amesema fumu hizo zitamuwezesha afisa kilimo na ushirika au mkuu wa wilaya kuwasiliana moja kwa moja na mkulima na kuhoji juu ya taarifa hizo ambapo ndipo ufuatiliaji utaanzia hapo.
aidha Mhe. Bashe amesema mfumo huo utasaidia upatikanaji wa taarifa muhimu na mawasiliano ya moja kwa moja na mkulima hivyo kuondoa tatizo la ukosefu wa taarifa baina ya serikali na wakulima pamoja na masoko.
Hata hivyo Mhe. Bashe ameziomba Halmashauri zote nchini kuweka malengo ya uzalishaji wa mazao kwa kila kila kata sambamba na ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao ya wakulima hasa kipindi hiki ambacho serikali inajitahidi kubadilisha kilimo kutoka cha kujikimu mpaka kilimo cha kibiashara.
Naye Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika (DAICO) wa Wilaya Chato Bw.Salimu Msuya amemuambia Naibu Waziri kwamba uzalilishaji umekuwa ukipungua maeneo mengi hapa nchini sababu ikiwa ni wakulima wengi kutofuata kanuni bora za kilimo (best agriculture practices) hivyo kuwa na mimea michache katika ekari moja.
“Utakuta mkulima anasema amelima ekari moja lakini kiukweli mimea iliyopandwa ni kidogo(plant population) kwa kutozingatia nafasi sahihi katika upandaji,kama ekari moja ingeingiza mimea 20,000 utakuta mkulima kapanda mimiea 7,000 hawezi kupata tija”Alifafanua Bw.Msuya.
Amesema hali ya uzalishaji katiika kilimo Wilayani Chato umeongezeka kutokana na wagani kusimiamia upandaji kwa kutumia mistari zoezi ambalo bado linaendelea.
Hata hivyo Bwana Msuya ameongezea kwamba kutozingati muda katika kilimo (agriculture timing) ni changamoto kwa wakulima walio wengi kwani hawalimi kwa na kupanda kwa wakati hivyo kujikuta wamepitwa na msimu wa kilimo na kusababisha mavuno kuwa kidogo.
Hata hivyo Bwana msuya amemuahidi Mhe Naibu waziri kwamba fomu hizo zitasaidia hata kuwajulisha wakulima kuanza kwa msimu,matumizi ya mbegu bora na utumiaji wa kamba katika upandaji.