Na.Alex Sonna,Dodoma
Leo ni oktoba 3 ,2019 ni siku ya kuadhimisha upingaji wa unywaji wa pombe duniani wananchi wameshauriwa kupunguza matumizi mabaya ya pombe ili kuepuka madhara kama ajali,ukatili wa kijinsi na magonjwa mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Dk Faustine Ndugulile alipo hudhuria maadhimisho hayo yaliyo andaliwa na shirika liliso la kiserikali linalo pinga matumizi mabaya ya pombe TAAnet ambapo amesema kuwa matumizi ya pombe yanasababisha madhara mengi katika jamii hususani vifo vya watu.
Aidha amezitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua watu wote ambao wanauza pombe kiholela na kufanya msako wa kukamata wote wanao uza pombe bila leseni.
Naye Anna Baraka Chaula Afisa Maendeleo ya jamii Kata Kising’a Mkoa wa Iringa amesema kuwa katika kata yake watu wengi walikuwa wanatumia muda mwingi kunywa pombe bila kufanya kazi za maendeleo huku akisema baada ya kupata elimu kwa sasa wamepunguza unywaji wa pombe.
TAAnet kwa sasa ina dhamira ya kutetea kushawishi sera na wafanya maamuzi kutengeneza kutekeleza sera ya Taifa ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe ambayo yatapunguza madhara ya kiafya na kijamii.