Home Michezo WACHEZAJI CHIPIKIZI WA MPIRA WA MIGUU KUTOKA AFRIKA WALIODHAMINIWA NA QNET WAHADITHIA...

WACHEZAJI CHIPIKIZI WA MPIRA WA MIGUU KUTOKA AFRIKA WALIODHAMINIWA NA QNET WAHADITHIA MAMBO WALIOYAONA MANCHESHTER CITY

0

Wachezaji chipikizi wa mpira wa miguu kutoka Afrika waliodhaminiwa na QNET wahadhithia mambo waliyoyaona Manchester City Watoto wamewakilishwa na mwandishi wa habari na Meneja wa PR wa QNET bwana Akoua Maxime.

Wachezaji chipikizi wa mpira wa miguu kutoka Afrika waliodhaminiwa na QNET wahadhithia mambo waliyoyaona Manchester City Mkurugenzi wa Masoko wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Ivory Coast, Mashabiki 3 wa mpira wa miguu waliodhaminiwa na QNET, Meneja wa PR wa QNET – SSA na Meneger wa Mambo ya Sheria wa QNET – SSA.

………..

Wachezaji wa mpira wa miguu chipukizi wa Afrika waliochaguliwa kutoka nchi za Ghana, Ivory Coast na Cameroun tarehe 31 August 2019, wameeleza fursa hiyo ya pekee na yenye kuhamasisha wakati wa mahojiano na vyombo vya habari jijini Abidjan, mji mkuu wa Ivory Coast. QNET iliwaalika waandishi wa habari katika mechi ya kupeana uzoefu kati ya Manchester City FC na Brighton & Hove Albion; Waandishi hao walitazama ligi ya mabingwa na kuzungumza na wachezaji chipukizi kutoka Afrika.  

QNET kampuni ya biashara ya mtandao inayoongoza ulimwenguni, kama sehemu ya jitihada zake za kuendeleza vipaji na kama namna ya kurudisha fadhila kwa jamii ambako inafanyia kazi, imedhamini wachezaji watatu vijana wa kiafrika kwenda kuhudhuria programu ya Lugha na Mpira wa Miguu ya kipindi cha msimu wa joto katika shule ya mpira wa miguu cha Manchester City jijini Manchester. Programu hii ilikua ya wiki mbili yenye lengo la kuhamasisha na kufundisha mpira wa miguu na kozi ya Lugha ya Kiingereza kwa wachezaji chipukizi wenye umri kati ya miaka 12-17. Programu hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 28 Julai mpaka tarehe 12 Agosti, 2019 katikati ya viwanja vya mafunzo vya timu ya Manchester City katika shule ya Mpira wa Miguu ya klabu ya City. 

Kwa mujibu wa Hamza Gaveh, wachezaji chipukizi kutoka Ghana walisema: “Ilikuwa ni moja kati ya wakati mzuri sana katika maisha yangu.  Nimepata fursa ya kupata mafunzo pamoja na klabu bora zaidi ya mpira wa miguu katika mashindano ya ligi za uingereza. Nimejifunza mengi kutoka katika vipindi vya mpira na kutoka katika vipindi vya Lugha ya Kiingereza. Nilikuwa kinara katika darasa langu la lugha ya kiingereza na katika michezo, nimejifunza zaidi kuhusu kufanya kazi kwa pamoja katika timu na mikakati ya kijihami.  Nimepata marafiki wapya kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Urusi na katika nchi za Sacandinavia.”

Baba Ndiaye kutoka Ivory Cost amesema: “Japo kuwa nimesafiri sehemu kadhaa kucheza mpira wa miguu, Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester City ni sehemu bora zaidi kati ya zote nilizowahi kwenda. Baada ya vipindi vya kuhamasisha tulivyovipata, sasa ninajihisi kwa kiasi kikubwa kwamba siku moja nataka kuchezea klabu ya manchester City. Ninafanya vizuri sana darasani na natumaini kufanya vizuri katika mpira wa miguu na kuchezea Ligi ya Maibingwa uingereza. 

Na Yvan Noh Nafeng kutoka Cameroun kwa furaha kubwa alisimulia:  “Sikuwahi kusafiri kwa ndege hapo awali na ilikuwa ni mara ya kwanza kupata hati ya kusafiria ya kimataifa. Tukio zima hili lilikuwa ni kitu kikubwa sana ambacho hakijawahi kutokea maishani mwangu. Nawafahamu wachezaji wengi chipukizi kutoka katika klabu yangu ya mpira wa miguu nchini Cameroun wanaotaka kuwa kama mimi, nimepanga kubakia na tabia njema na kuwa makini.  Vile vile ninapanga kuwafundisha wenzangu baadhi ya masomo ya mpira wa miguu niliyojifunza”.

Akiongea katika sherehe, Bwana Rajesh Rao, Mkurugenzi wa Mkuu wa QNET wa Mahusiano ya Kimataifa, alisema. “Programu hii ni sehemu ya jitihada za QNET za kuendeleza vipaji, kurudisha kwa jamii ambako tunaendesha shughuli zetu pamoja na jamii kwa ujumla.  Tunaamini kwamba fursa waliyopata kutoka Klabu ya Manchester City FC imewahamasisha vijana hawa kutafuta viwango vya juu katika maisha yao”.

Akiongea kuhusu ushirikiano kati ya Manchester City, QNET na programu ya mpira wa miguu, Bwana Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET kanda ya Afrika, amesema “QNET ni biashara ambayo inaamini na kudumisha uendelevu. Tunaamini katika kuendeleza na kukuza vipaji katika ngazi zote.  Udhamini wa Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester City kama mshirika wa mauzo ya moja kwa moja na mdhamini wa lebo za mikononi (Sleeve Sponsor) ni moja kati ya jitihada zetu katika mpira wa miguu pamoja na hamasa ambayo mpira huo unaambatana nao duniani kote. Kupitia Ushirikiano huu, tumepata fursa ya kupeleka watoto wanaotokea katika familia zenye kipato cha chini Afrika kwenda katika klabu za mpira wa miguu na shule ya lugha ya kiingereza jijini Manchester; jambo hili kweli limebadilisha maisha ya watoto hawa,  Watoto tunaowasherehekea leo ni matunda ya ushirikiano huu. Tunatumaini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja na kutafuta njia mpya za kibunifu za kushirikiana na kuwafikia wadau wetu wote.”

QNET inaendelea kupanua uwepo wake katika sehemu mbalimbali katika bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambako inatoa fursa za ujasiriamali kwa watu na kuwasaidia kubadilisha maisha yao kuwa bora zaidi. Mbali na ushirika katika michezo, QNET vile vile ni kampuni ambayo imewekeza katika kuwajibika kwa jamii, kurudisha na kutoa kwaajili ya manufaa ya jamii na jambo hili linafanyika katika maeneo yote ambako QNET inaendesha shughuli zake. Katika mwezi Novemba mwaka  2018, Kampuni ya QNET ilitunukiwa tuzo ya e-Commerce CSR Company kuwa ni kampuni bora ya biashara ya mtando kwa mwaka huo, ambayo ilitolewa na Kituo cha Uwajibikaji wa Mashirka kwa Jamii cha Afrika Magharibi (Centre for Corporate Social Responsibility West Africa.)