Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Pwaga Wilayani Mpwapwa Jimbo la Kibakwe akizungumza na wanafunzi na wananchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akipanda mti eneo la ya Sekondari Pwaga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa masomo ya sayansi kwa vitendo katika Shule ya Sekondari Pwaga.
Afisa Elimu wa Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Nelson Milanzi akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene kuzungumza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akitoa cheti kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi kwa upande wa wavulana Elibariki Muzaye.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio kwenye mahafali ya kumaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Pwaga wilayani Mpwapwa ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akizungumza kwenye mahafali ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Pwaga Wilayani.
Wahitimu wa kidato cha nne Shule ys Sekondari Pwaga wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene.
……………………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene amehimiza matumizi ya nishati mbadala kupikia ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
Mhe. Simbachawene ametoa rai hiyo wakati akihutubia wanafunzi na wananchi katika mahafali ya kumaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Pwaga wilayani Mpwapwa.
Aliwataka wananchi kuacha mara moja kukata miti kwa ajili ya kuni au mkaa na kusema kuwa vitendo hivyo huchangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi.
Mhe. Simbachawene ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kibakwe alisema kuwa wakati umefika sasa kwa wananchi kuanza kutumia gesi katika shughuli za kupika hivyo kuepuka matumizi ya mkaa au kuni ambayo huchangiwa kwa kiasi kikubwa na ukaaji wa miti.
“Tukiyachezea mazingira tunachezea uhai wetu na ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa unaishia kusababisha kumalizika kwa maeneo yenye miti mikubwa na wengine wanakata miti kwa kiwango kikubwa hata tukae miaka mingi hatutakuja kupata tena miti kama hiyo,” alisisitiza.
Aidha, Waziri Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe wilayani humo aliwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao na kuwatia moyo.
Pia alikemea tabia ya baadhi ya wanafunzi wa kike kuanza kushiriki katika vitendo vya ngono kabla ya umri na kuwataka kuzingatia masomo na hivyo kufikia malengo yao na kuwaonya wazazi wanaoficha wahusika wa mimba hizo.
Alionya tabia ya baadhi ya wanaume wanaowarubuni wanafunzi wa kike na kushiriki nao ngono vitendo vinavyosababisha kuwapa mimba na hivyo kukatisha masomo yao.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Nelson Milanzi alitoa mwito kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla kutunza mazingira.
Afisa Elimu huyo aliwataka kuunga mkono juhudi za Ofisi ya Makamu wa Rais na Serikali kwa ujumla kutunza mazingira na kupanda miti kwa wingi.