NJOMBE
Shirika lisilo la kiserikali la Muungano wa Jamii Tanzania MUJATA limefanikiwa kuzikutanisha pamoja familia mbili zilizokuwa na uhasama mkubwa kwa zaidi ya miaka 15 zinazoishi mtaa wa kikula halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe ambao ulifikia hatua ya kutishiana na maisha kwa madai ya uvamizi wa ardhi.
Familia hizo zimekuwa kwenye mgogoro mzito zaidi ya muongo mmoja na nusu, licha ya kufikishana katika vyombo vya sheria na usuluhishi ikiwemo mahakama na mabaraza ya kata bila ya mafanikio kwakuwa kila upande una imani kwamba ndiyo mmiliki harari wa eneo hilo ambalo linadaiwa kuuzwa na familia ya mzee Simon Mgindu kwa nyakati tofauti katika familia mbili tofauti .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu uharari wa umiliki katika kipande hicho cha ardhi Mzee Maltin Mgeni maarufu rodirofa anasema yeye ndiyo mmiliki harari kwa kuwa aliuziwa eneo hilo 2004 kwa gharama ya elfu 80 na Mjomba wa familia hiyo huku nae Emmanuel Kunyumba akidai alinunua eneo hilo sh.laki 410 mwaka 1995 kwa marehemu Atanas Mgumba ambaye ndiye alikuwa mmiliki harari wa eneo hilo na kuomba haki itendeke kumpata mmiliki sahihi.
Mgogoro huo ambao umegonga mwamba katika vyombo vya sheria tangu 2009 una amriwa na Shabani Kusaga ambaye ni mjukuu wa familia ya Ngunda ambaye anasema kipande hicho cha ardhi kiliuzwa na mjomba wake 2004 kwa Maltini Mgeni maarufu rodirofa .
Kwa upade wake mwenyekiti wa mtaa wa Kikula Joseph Makweta maazimio ya mwisho yaliyofikiwa ofsini kwake ni kwamba mzee kunyumba anapaswa kuwa mmiliki kwa kuwa alimlipa fidia ya laki mbili mzee Maltin Mgeni ili kulipata eneo .
Mara baada ya kusikia hoja kutoka pande zote zinazosigana, familia na uongozi wa mtaa wa Kikula ndipo timu ya usuruhishi wa migogoro kutoka taasisi ya muungano wa jamii Tanzania MUJATA ikiongozwa na Sebastian Kibiki ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya fedha taifa MUJATA na Benjamini Msafiri ambaye ni mwenyekiti wa kanda ya nyanda za juu kusini wanatoa ushauri wao.
Kisha wanafanikiwa kuwaunganisha tena na kupeana mikono hatua ambayo imeashiria udugu kurejea tena