Na Mwandishi Wetu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara amefurahishwa jinsi Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam lilivyoweza kukuza mila na desturi za Mwafrika.
Akizungumza mara baada ya kutembelea katika uwanja wa Taifa leo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa amefurahishwa jinsi walivyoweza kusogeza ajenda ya Biashara nchini.
“Nafurahi kwamba maonesho haya yameshirikisha watu wote, nimefurahi kuone watu wenye ulemavu wanatengeneza bidhaa nzuri ambazo zinawapatia kipato,” amesema.
Amesema kuwa amefurahiswa kuona Mila na desturi zinafanana, ukiachana masuala madogomadogo tunaweza kushirikiana kwa karibu ili kujenga uchumi mkubwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Nimetembelea banda la Jumuiya ya Afrika Mashariki na nimeangalia takwimu za nyuma kidogo za biashara za nchi wanachama zinaonesha biashara inaongezeka, kwa kiasi kikubwa Sana, kwa hiyo jukumu kubwa ni kujenga amani ili kujenga uchumi wa nchi zetu,” amesema.
Ameongeza kuwa Tamasha la JAMAFEST ni fursa kubwa kwa wa EAC, kwa hiyo tunaweza kuangalia utaratibu wa kupunguza muda wa miaka miwili ili kuwawezesha watu wetu kufanya biashara na kupanua soko baina ya nchi Wanachama wa EAC.
Mhandisi Stella Manyanya bidhaa zinazopatikana hapa JAMAFEST zinatufundisha kuwa Nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla tuna vipaji vikubwa sana kutoka kwenye Sanaa na Utamaduni wetu.
Ngoma kutoka nchini Tanzania ikiburudisha katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akingalia burudani ya ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Watoto wa kitanzania akionyesha umahili wa kupiga ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Burudani ikiendelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (kulia) akingalia bidhaa wa wajasiliamali wa jumuiya ya Afrika Mashariki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (katika) akingalia burudani ya mchezo wa bao katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa manyoka nyoka ukiendelea.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili toka kulia) akifuatilia burudani ya ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.