Mkurugenzi wa Kituo cha NIMR_Mbeya, Mtafiti Mkuu wa Mradi wa Smert (Tanzania_Uk) Dkt.Nyanda Ntinginya akiongea na wanahabari katika mkutano wa mwaka wa pili wa Smert project uliofanyika katika ofisi za TMDA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kuratibu na kukuza utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt.Paul Kazuoba akizungumza na wanahabari katika mkutano wa mwaka wa pili wa Smert project uliofanyika katika ofisi za TMDA jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watafiti pamoja na wakurugenzi kutoka katika taasisi mbalimbali wakipata picha ya pamoja katika mkutano wa mwaka wa pili wa Smert project uliofanyika katika ofisi za TMDA jijini Dar es Salaam.
************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Watafiti wa dawa za binadamu wamehimizwa kufanya tafiti ambazo zitasaidia uzalishaji wa dawa ambazo zitamlinda mtumiaji na kuepusha athari zinazoweza kujitokeza baada ya matumizi
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi wa kuratibu na kukuza utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt.Paul Kazuoba katika mkutano wa mwaka wa pili wa Smert project uliofanyika katika ofisi za TMDA jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Dkt.Kazuoba amewataka Wananchi kujijengea utaratibu wa kuuliza kama tafiti za afya zimepitia utaratibu hivyo taasisi ndogondogo zinazofanya utafiti wa afya zijijengee uwezo wa kuweza kutathimini maadili ya tafiti zenyewe.
Lengo kubwa la kuwa na Smert project ni kuhakikisha Mwananchi analindwa katika usalama wake kwenye matumizi ya dawa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha NIMR_Mbeya, Mtafiti Mkuu wa Mradi wa Smert (Tanzania_Uk) Dkt.Nyanda Ntinginya amesema kuwa mradi huo ulianzishwa kwa malengo ya kuimarisha utendaji kazi wa kamati za naadili za taasisi pamoja na utendaji kasi wa kamati za kikanda za utafiti.
“Kabla ya mradi huu atujafanya kulikuwa na changamoto ya muda mrefu kutumiwa kabla ya mradi kuruhusiwa kwenda kufanyiwa utafiti”.Amesema Dkt.Ntinginya.