Jeshi la polisi limekamata magendo ya kahawa yakisafilishwa kwenda uganda katika halmashauri ya wilaya ya bukoba mkoani kagera.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa kituo cha polisi Bukoba mkoani kagera SSP Babusanare Ally amesema kuwa mnamo tarehe 24 Sep.mwaka huu majira ya 22:10 askari waliokuwa doria walipa taalifa kuwa gari lenye usajili NO.T.205 DHX Mitsubishi Fuso kwa kosa la kusafirisha kahawa bila kibali ambapo watuhumiwa ni Sadick Charles, Jonizius Gerad na Lazaro Mdesa.
Pia amesema kuwa magendo hayo ya kahawa yamekamatwa maeneo ya Bulila, Kata Kemondo, Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera ambapo yalikuwa yanapitia Mwalo wa Bilolo kemondo kuelekea nchini Uganda.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawilo amesema kuwa magendo yaliyokamatwa ni magunia 115 huku Dereva wa Gari hilo ameweza kutoroka na bado jeshi la Polisi linamtafuta.
Pia ameongeza kuwa kutokana na juhudi za jeshi la polisi watuhumuwa watatu wamekamatwa huku akimtaja askari aliyeweza kuendesha gali hilo mpaka kituo cha poli ambaye ni Askari No. G.9158 PC Joseph na kusema kuwa watuhumiwa wote wamefikishwa kituo cha polis Bukoba kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Vilevile amezipongeza juhudi za jeshi la polisi na kusema kuwa lihakikishe kila aliyehusika katika kusafirishwa kwa magendo hayo ya kahawa sheria inafuata mkondo wake na kuwawajibisha ipasavyo.
“Dolia hii iwe endelevu hasa katika maeneo mnayoyadhania yanaweza kuwa na makosa ili kutetea juhudi za Rais wetu Mh.Dk.John Pombe Magufuli kutokana na makosa yanayojitokeza katika kahawa maana watu kama hawa wanarudisha maendeleo nyuma hawatakiwi kuachwa kabisa” Alisema Kinawilo.