Home Mchanganyiko MKULIMA AISHUKURU SERIKALI

MKULIMA AISHUKURU SERIKALI

0
Mzee Musa Ndembo akitia saini ya dole gumba kukiri kupokea fedha zake Leo Jumatano Septemba 25, 2019 tukio likishuhudiwa na Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu, Mtendaji kata Michenjele Shazir Hamis, Mke wa Mzee Ndembo (hayupo pichani) na Viongozi wa Michenjele Amcos (hawapo pichani) katika ofisi ya Mtendaji kata Michenjele
…………………
Na Mwandishi wetu Mihambwe
Mkulima wa Korosho mkazi wa Kata ya Michenjele Mzee Musa Chuma Ndembo ameishukuru Serikali kwa kusimama kidete hadi kuhakikisha analipwa madeni yake. 
Mzee Ndembo ameyasema hayo mara baada ya kulipwa madeni ya fedha za Korosho aliyokuwa akidai kwa chama cha msingi cha Michenjele ambacho alisumbuka nacho kwa zaidi ya miezi 5 akitafuta haki yake na kutokupata hadi pale suala lake alipolipeleka ngazi za Serikali.
“Nimeteseka kwa zaidi ya miezi mitano nikikidai  chama cha msingi pasipo mafanikio lakini ndani ya wiki moja tu tangu nilipofikisha suala langu kwa Afisa Tarafa Mihambwe nimelipwa fedha zangu. Naishukuru sana sana Serikali.”amesema Mzee Ndembo
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ya fedha Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ambaye alikuwa shuhuda na msimamizi wa haki ikitendeka amesema  kazi ya Serikali ni kuhakikisha kuna haki na usawa ndani ya jamii na hakuna Mtu yeyote yule atakayeonewa.
“Serikali ipo na inaendelea kusimamia haki ikitendeka kwa jamii. Natoa Rai kwa Viongozi wa vyama vya Msingi kuacha kuwasumbua, kuwanyanyasa na kutaka kuwadhulumu Wakulima. Nawasisitiza Amcos wote wenye madeni ya Wakulima mfanowe Mzee Ndembo na wengineo wawalipe mara moja kujiepusha matatizo na vyombo vya sheria.” Alisisitiza Gavana Shilatu
Makabidhiano hayo yamefanyanyika ofisi ya Mtendaji kata Michenjele na kuhudhuliwa na chama Cha Msingi, Mkulima Mzee Ndembo na Mkewe pamoja na Mtendaji kata