********************************
Na Silvia Mchuruza.
Kagera.
Kufuatia uchaguzi wa serikali za mitaa mkoani kagera unaotegemea kuanza kufanyika tarehe 24 Nov. 2019 viongozi wa upinzani wameuomba uongozi kufanya uchaguzi wa haki na kutumia ustaharabu hili kutofanya tena makosa yaliyojitokeza siku za nyuma.
Hayo yamesemwa na baadhi ya viongozi wa vyama pinzani akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo CHADEMA manispaa ya bukoba Ndg.Victor Sherejey ambapo amelaani vikali mgogoro uliojitokeza uchaguzi uliopita kutoka kata ya Hamgembe, na Kagondo zilipo katika halmashauri ya Bukoba manispaa mkoani humo.
Nae msimamizi wa uchaguzi wa serikali katika halmashauri ya Bukoba manispa Ndg.Richard Masamilo Mihayo amesema kuwa uchaguzi wa awamu hii utakuwa ni uchaguzi wenye haki ambapo utahusisha kata 66 kutoka kata zote za halmashauri hiyo.
Aidha amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo kuwa waaminifu na waangalifu katika kazi wanayoenda kuifanya hili kuleta amani pamoja na hayo ameyata matarajio ya watu wanaotegemewa kujiandikisha katika uchaguzi huo.
“Lengo la kuwakutanisha wadau hawa wa uchaguzi ni kuwaelekeza jinsi ya kusimamia uchaguzi uende vizuri lakini kuna kata 66 pia wapo hata wasimamizi wa jimbo na wasimamizi ngazi ya kata na watu ambao tunategemea kujiandikisha ni zaidi ya wananchi elf 83 ambapo uandikisha utachukua siku 7 kuanzia tarehe 8 hadi 14 mwezi wa kumi mwaka huu” alisema Ndg.Richard Masamilo.
Pia Masamilo ameongeza kuwa kila mwananchi ambae alihama makazi, aliyepoteza kitamburisho chake cha awali, anaeona taarifa zake zilimosewa, mwenyekitamburisho kilicho haribika wote hao wanatakiwa kujiandikisha upya katika daftali la kudumu la mpiga kura.
Vilevile nae katibu tawala wa wilaya hiyo DAS Kadole Kilugala ambae ndiye kiongozi wa ulinzi na usalama katika uchaguzi huo ameomba ushirikiano kwa wadau na kuwataka kuwa watiifu na waadili katika shughuri hiyo hili kuleta amani ya chaguzi hizo.