Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya udhibiti wa Madawa ya Kulevya James Kaji akiongea na Wanahabari katika ofisi za Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam leo.
NA EMMANUEL MBATILO
****************************
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya kwa kushirikiana na jeshi la polisi linamshikilia alirkuwa Afisa Usalama wa Shirika la Posta Tanzania Bw.George Arsein Mwamgambe kwa tuhuma za kusafirisha madawa ya kulevya kwa njia ya Posta.
Ameyasema hayo leo Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya udhibiti wa Madawa ya Kulevya James Kaji katika mkutano wa Wanahabari katika ofisi za Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari Kami.Jen.Kaji amesema kuwa wamemshikilia mtuhumiwa huyo ambaye wawli alitoweka kufuatia mahojiano yaliyokuwa yakiendelea dhidi yake pamoja na watuhumiwa sita (6) wanaohusishwa na dawa za kulevya aina ya Heroin uchunguzi wake um ekamilika na watafikishwa mahakamani.
“Uchunguzi wa kimaabara kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ulithibitisha, majani hayo yana kemikali aina ya cathinone ambayo inapatikana kwenye mmea wa mirungi (Cath edulis)”.Amesema Kami.Jen.Kaji.
Aidha Kami.Jen.Kaji amesema kuwa taarifa za awali zilibaini kuwepo kwa usafirishwaji wa kiasi kikubwa cha dawa za kulevya aina ya mirungi kutoka nchini kwenda nchi za Ulaya kwa njia ya posta, zikiwa zimepewa majina bandia, ambapo ilibainika dawa hizo ziliingizwa nchini kutoka nchini Ethiopia kama majani ya mlonge na kufungwa upya kisha kusafirishwa tena kwenda nchi za Uingereza, Canada,Ufaransa na nchi nyingine za Ulaya.
“Awali vifurushi hivyo vilikuwa vikisafirishwa kupitia posta ya Dar es Salaam na sasa vimekamatwa vikisafirishwa kupitia Posta Jijini Arusha”. Amemaliza kwa kusema Kami.Jen.Kaji.