KUPATIKANA NA SARE ZA JESHI LA POLISI NA MALI ZA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia KELVIN MANYUSI [32] fundi umeme, mkazi wa Teku Jijini Mbeya akiwa na sare za Jeshi la Polisi ambazo ni TT 2 kitengo cha ffu, koti la mvua rangi nyeusi pamoja na mkanda wa filimbi ambavyo ni mali za Jeshi la Polisi Tanzania.
Mtuhumiwa alikamatwa Septemba 20, 2019 saa 15:30 alasiri katika msako uliofanyika huko Mtaa wa Ngosi, Kata ya Mwakibete, Tarafa ya Iyunga, Jiji la Mbeya.
Pia mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa na vifaa vya kuvunjia ambavyo ni panga, bisibisi pamoja na tindo. Aidha mtuhumiwa baada ya kupekuliwa nyumbani kwake alikutwa na mali mbalimbali zidhaniwazo kuwa za wizi ambazo ni
- “TV” 2 aina ya “Samsung” nchi 32, “Aborder” nchi 32,
- “System Case” mbili aina ya “Dell na Hp”,
- “Keyboard” 1 aina ya “Hp”,
- “Receiver” tatu za vinga’muzi vya “Dstv”, Azam na “Startime”,
- Speaker” mbili za “Seapiano” na “Topsonise”,
- Simu za Mkononi 9 kati yake “Smartphone” tatu na sita za kawaida 6,
- “External” 4,
- Kamera moja aina ya “Ricoh”,
- “Remote control” 14,
- “Switch ya Internet” 1,
- “Dryer” mbili moja ya mkono ndogo na kubwa,
- Jiko la umeme 1,
- Amplifier na Equalizer 1 aina ya metal,
- Twitter 7,
- mouse 1,
- Rasta bunda 7 za kusukia nywele bandia,
- Uzi bunda mbili za kushonea,
- Mashine ya Blenda nyeupe ,
- Saa 3,
- Deki 1 aina ya LG,
- Mitungi 2 ya Gesi aina ya Oryx,
- Jiko la Gesi 1 la plate mbili.
Upelelezi unaendelea.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WATATU KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NYARAKA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wanawake watatu kwa tuhuma za kughushi nyaraka mbalimbali kwa lengo la kupata mkopo katika Benki ya Posta Tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya.
Watuhumiwa wamekamatwa Septemba 19, 2019 saa 16:00 jioni huko Benki ya Posta iliyopo maeneo ya Mwanjelwa Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa watuhumiwa wameghushi majina yao halisi kwa lengo la kupata mkopo kwa njia ya udanganyifu na kukwepa kuonekana kuwa wanadaiwa na taasisi nyingine za fedha.
Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
- FARIDA YESSAYA @ TUMPALE [23] Mfanyabiashara na Mkazi wa Uyole ambaye ametengeneza nyaraka zake kwa kutumia jina la mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aitwaye CAREN ZABRON @ BANDARI.
- ASHA HARZINA @ NAMWENE [29] Mfanyabiashara na Mkazi wa Uyole ambaye ametengeneza nyaraka zake kwa kutumia jina la mama yake mzazi ambaye ni marehemu aitwaye ZAITUNI ABIANI @ BAKILI.
- REBECCA YESSAYA @ MSIGALA [47] Mfanyabiashara na Mkazi wa Uyole ambaye ni Mwenyekiti wa Kikundi na alithibitisha majina hayo huku akijua sio majina yao halisi waliyotumia kuchukua mkopo katika taasisi ya fedha – FINCA.
Watuhumiwa kwa pamoja waliomba mkopo wa shilingi milioni mbili na laki tano [2,500,000] na walitegemea kupewa mkopo huo tarehe 19.09.2019 ila kabla ya kupewa fedha hizo Jeshi la Polisi liliweza kubaini kuwa watuhumiwa wametumia majina yasiyo yao ili kukwepa kurejesha fedha hizo. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa Mahakamani.
KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
Mnamo tarehe 21.09.2019 majira ya saa 00:15 usiku wa kuamkia leo huko nyumba ya kulala wageni iitwayo Gaga iliyopo Mtaa na Kata ya Bagamoyo, Tarafa ya Tukuyu Mjini, Wilaya ya Rungwe na Mkoa Mbeya. Polisi walimkamata BONNY BONNY BANDA [35] raia na mkazi wa Nchni Malawi akiwa ameingia Nchini bila kibali. Upelelezi unaendelea.
KUPATIKANA NA BHANGI NA POMBE MOSHI.
Mnamo tarehe 19.09.2019 majira ya saa 01:50 usiku huko Kijiji cha Izumbwe kilichopo Kata ya Igale, Tarafa ya Usongwe, Wilaya Mbeya Vijijini, Mkoa Mbeya. Askari Polisi walimkamata AHAZI ISSA @ MAPOGELO [31] Mkazi wa Izumbwe akiwa na bhangi kilo 2 na gramu 220 pamoja na Pombe Moshi ujazo wa lita moja [01] ndani ya nyumba yake. Mtuhumiwa ni mtumiaji na muuzaji wa bhangi na Pombe Moshi. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa Mahakamani.