**********************************
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU imewataka watanzania kwa ujumla kutumia uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na vijiji vizuri pasipo kupokea RUSHWA kwa mgombea yoyote ili kuweza kuchagua viongozi bora ambao watawaongoza na kutimiza malengo yao.
Akizungumza na wanagabari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,Brig.Gen.John Mbungo amesema kuwa taasisi hiyo imedhamiria kuwaelimisha wananchi ili waweze kuchagua viongozi ambao wataendelea yale yote mema yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano.
“Ni dhamira ya TAKUKURU kuona kwamba umakini unakuwepo kuchagua viongozi waadilifu, wazalendo na wasiojihusisha na vitendo vya Rushwa unazingatiwa na watanzania wote katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na vijiji utakofanyika Novemba mwaka 2019”. Amesema Brig. Gen. Mbungo.
Aidha,Brig.Gen.Mbungo amesema kuwa uelimishaji unafanyika nchi nzima ,jitihada zimefanyika ili kuzitumia Rdio za jamii ambazo zipo katika mikoa mbalimbali nchini ambako TAKUKURU inazo ofisi zake.
“Njia nyingine ya uelimishaji tunayoitumia ni kupitia maonesho ya filamu katika mikusanyiko mbalimbali ikiwemo mikesha ya mbio za Mwenge wa Uhuru unaokimbizwa nchi nzima hadi Oktoba 14,2019.