NJOMBE
Kufuatia ongezeko la wimbi la watumishi wa umma kustaafu kwa hiari kwa madai ya kujawa na hofu ya kuanza kutumika kwa sheria mpya ya hesabu za makadilio ya kikokotoo inayotarajiwa kuanza kutumika ifikapo 2023, Hatimae rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUKTA Tumaini Nyamhokya ametolea ufafanuzi suala hilo na kuwatoa hofu wanafanyakazi.
Akiwatoa hofu katika mkutano wa mwaka ambao umekutanisha wanachama wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa mkoani Njombe Tumaini Nyamhokya ambaye ni rais wa TUKTA Tanzania amesema kustaafu kwa hiari kupo kwa mujibu wa sheria na kuhusu hofu ya mabadiliko ya kikokotoo hadi sasa imeundwa timu kutoka kwa wafanyakazi na timu ya serikali kwa lengo la kuandaa kikokotoo kitakachokuwa rafiki kwa wastaafu na mifuko ya hifadhi za jamii.
Mbali na suala hilo rais huyo pia amezungumzia changamoto ya kiwango kikubwa kisichowiana cha kodi ya mshahara(pay as you earn) pamoja na madaraja zinavyoshughulikiwa na serikali.
Awali akifngua mkutano huo utakaofanyika wa siku mbili mgeni rasmi ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amewataka watumishi kuondoa hofu ya kuishi maisha magumu mara baada ya kustafu kwa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo.
Benedeta Mathias,Festo Mbakilwa na Agness Masasi na ni miongoni mwa wanachama zaidi ya elfu 20 wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGU ambao wanasema kodi ya mshahara bado kubwa ukilinganisha na ukali wa maisha huku pia suala la kustafu kwa hiari likishika hatamu.