*********************************
NJOMBE
Mkulima mmoja katika kijiji cha Itulike halmashauri ya mji wa Njombe anaefahamika kwa jina la Steven Mlimbila ambaye amekulia katika mazingira magumu akilelewa na bibi kabla ya kujikita katika kilimo na kuwa milionea kupitia kilimo, ameonyesha hisia zake baada ya mwenge wa uhuru kukagua shamba lake na kutambua jitihada zake ambazo zimesaidia kutoa ajira kwa zaidi ya watu 37.
Steven Mlimbila amedaiwa kuwa miongoni mwa wakulima wachache wenye mafanikio makubwa katika kilimo cha parachichi mwaka jana alifanikiwa kushinda tuzo ya mkulima bora wa kanda ya nyanda za juu kusini na mkoa wa Njombe kutoka na kufanya kilimo bora huku akiwa amefanikiwa kajiri watu wengi kwa ujira wa siku wiki na mwezi.
Akizungumza jitihada ambazo amezichukua hadi kufikia mafanikio katika kilimo Mlimbila amesema alianza shughuli hiyo katika mazingira 2010 na kwamba kutokana na uhakika wa soko la ndani na nje la matunda hayo yanayotumika kutengeneza mafuta, dawa na chakula amefikia hatua ya kuwa mkulima mwenye uwekezaji wa zaidi ya mil 200 shambani.
Mara baada ya kukagua shamba la mfano la parachichi la mkulima huyo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Mzee Mkongea Ally analazimika kumwagia sifa mkulima huyo kwa kudai kwamba uwekezaji wake ambao umetoa ajira kwa vijana umetoa fursa kwa wengine kuajiriwa na kujifunza kwake kilimo hicho
Nao baadhi ya wafanyakazi wa kudumu na vibarua ambao wamepata ajira katika mashamba ya mkulima huyo akiwemo Fraviana Mgimba na Anord Steven wanasema awali maisha yao yalikuwa duni zaidi na kwamba mapema baada ya kuajiriwa na mkulima huyo wakafanikiwa kutunza familia na wazazi wao kwa kuwa wanalipwa kwa wakati.
Mwenge wa uhuru ukiwa halmasahuri ya mji wa Njombe umekagua miradi 12 yenye thamani ya bil 6.2.