Rais wa Shirikisho la Filamu nchini Tanzania TAFF Bw. Saimon Mwakifwamba akizungumza wakati shirikisho hilo lilipotambulisha rasmi mchakato wa kusambaza rasimu ya katiba ya filamu kwa wasanii na wadau wa tasnia ya filamu.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika ofisi za bodi ya filamu jijini Dar es salaam
……………………………………….
BODI ya filamu nchini kwa kushirikiana na shirikisho la filamu nchini (TAFF) wameanza wa mchakato wa kusambaza rasimu ya katiba ya filamu kwa wasanii na wadau wa tasnia ya filamu.
Akizungumza na waandishi wahabari Kaimu Katibu wa bodi ya filamu Kiago Kilonzo amesema rasimu hiyo ikikamilika itaweza kufanya ya utetezi wa tasnia ya filamu pamoja na wasanii wenyewe.
Bodi inaunga mkono shirikisho la filamu kwa kuanza mchakato huo wakusambaza rasimu ili kufanikisha kupatikana kwa katiba itakayowaongoza wasanii kisheria kwenye kazi za kisanaa.
“Tutaendelea kuunga Mkono juhudi zinazoendelea na shirikisho Hilo kuanzia kusambaza katika kila kona ili kupata usawa wa maoni kutokana na zoezi hilo kufanyika kwa uwazi bila upendeleo,”
Kwa upande wake Rais wa shirikisho la filamu nchini (TAFF) Simon Mwakifamba ameeleza kuwa baraza la sanaa (BASATA) pamoja na bodi ya filamu ndio mihimili mikuu kiutendaji wa kazi za Sanaa.
Aidha Mwakifamba amefafanua zaidi kuwa shirikisho hilo linajivunia kuipigania sera ya filamu tangu 2014 na Serikali imeshatoa ahadi ya kabla kuisha kwa mwaka huu itafanikisha kupatikana kwa katiba .
“Tumeazimia kuwa zoezi hili la ukusanyaji maoni litakua na takribani muda wa mwezi mmoja ikiambatana kusambazwa kwa njia mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii Facebook,magazeti pamoja blogs ,”
Pia Mwakifamba ametoa wito kwa wadau wote wenye nia njema kutoa mawazo yao ili kuujenga umoja huu wenyewe Tasnia ya filamu nchini ili kuijenga tasnia yenye mchango wa kiuchumi kwenda katika uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.