Na Silvia Mchuruza;
Kagera;
Shirika lisilo la kiserikali mkoani kagera “TEKLA KAGERA” limetoa mafunzo kwa wajumbe wa WDC na kamati za jamii juu ya ujumuishwaji kwa watu wenye ulemavu kika jamii xinazowazunguka.
Mafunzo hayo yametolewa na mratibu wa shirika la TEKLA KAGERA Bw.Mgisha Kasaju ambapo amewataka wajumbe hao kuutumia vizuri mfumo wa elimu jumuishi na kuifanya jamii kutambua ujumuishwaji wa watu au watoto wenye ulemavu.
Hata hivyo mafunzo hayo yameudhuriwa na wajumbe kutoka serikali ya mkoa na ngazi za chini ambapo walihudhuria maafisa elimu kata na wilaya madiwani, watendaji wa kata 5 ambazo zipo katika mpango huo wa kutoa elimu jumuishi pamoja na muwakili kutoka kalika ofisi ya kaimu mganga mkuu wa mkoa kagera.
Vile vile Bw. Mgisha ameitaka serikari ya mkoa kutambua elimu jumuishi kwa watoto wenye ulemavu na haki za watoto wenye ulemavu mashuleni.
“Shule za kawaida zinaweza kuwa jumuisha watoto wote mashuleni na kuwawezesha walimu kuwa nauelewa zaidi juu ya elimu jumuishi na kuungwa mkono kwa mpango wetu tunaoufanya sisi kama TEKLA KAGERA” Alisem Bw.Mgisha.
Pia ameyataja matarajio yao waliyo nayo ni kuandaa semina na wadau juu uwezeshwaji wa elimu jumuishi katika mashule ili kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupata haki zao za msingi.
“Zaidi ya wazazi 375 wameishanufaika na elimu jumuishi kwa watu wenye ulemavu na zaidi ya wajumbe 45 wamenufaika kwahiyo tunaratajia jamii kwa ujumla kuelimika na mpango wa elimu jumuishi kupitia TEKLA KAGERA”Alisema Bw. Mgisha.
Hata hivyo Bw. Mgisha maeongezea na kusema kuwa zaidi ya shule 6 zimenufaika na mpango huo kutoka katika kata 5 ba zaidi ya wanafunzi 420 wamenufaika na kuzijua haki zao za msingi.
Sambamba na hayo nae kaimu Mwenyekiti wa shirika la TEKLA KAGERA Bi.Analise Lubago(mlemavu wa macho) amewataka wajumbe kuzijua sheria za watu wenye ulemavu hili kuelimika zaidi na elimu jumuishi hili kuishirikisha jamii kwa ujumla.
” Ulemavu ni kila mtu maana hakuna anae jua keshi yake ni vyema kuzijua sheria na kuwapa elimu zaidi kuwa na muitikio kwa walimu hili kuwawezesha wanafunzi wenye ulemavu kupata mahitaji yao ya msingi”