Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri anayeshuhulikia Mashirika yanayomilikiwa na Serikali ya Indonesia Bibi.Rini M.Soemarno (kulia) wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe wake.[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waziri anayeshuhulikia Mashirika yanayomilikiwa na Serikali ya Indonesia Bibi.Rini M.Soemarno (wa pili kulia) leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waziri anayeshuhulikia Mashirika yanayomilikiwa na Serikali ya Indonesia Bibi.Rini M.Soemarno (wa pili kulia) leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake.
…………..
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameipongeza azma ya Serikali ya Indonesia ya kuja kuekeza Zanzibar kupitia Makampuni na Mashirika yake ya Umma kutokana na fursa zilizopo hapa nchini.
Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri anayeshughulikia Mashirika yanayomilikiwa na Serikali ya Indonesia Bi Rini Mariani Soemano.
Katika maelezo yake, Rais Dk. Shein alimueleza Waziri Soemarno kuwa azma hiyo ya Serikali ya Indonesia ni hatua moja wapo ya kukuza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano ulioasisiwa na waasisi wa Mataifa hayo akiwemo Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Soekarno Hatta Baba wa Taifa la Indonesia
Rais Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kushirikiiana na Makampuni na Mashirika yote ya Umma ya Indonesia yalioonesha azma ya kuja kuekeza hapa Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo.
Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alieleza kuwa ujio wa Waziri Bi Rini Soemarno unaonesha mwanzo mzuri wa mashirikiano hayo katika kuendeleza sekta mbali mbali za maendeleo zikiwemo uwekezaji, biashara, utalii, kilimo, miundombinu na nyengienzo.