Home Mchanganyiko OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI YATOA MAFUNZO KWA WAHARIRI WA VYOMBO...

OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI YATOA MAFUNZO KWA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI

0

Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Esther Hellen Jason akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa wahariri, Dar es Salaam kushoto ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelice Mafumiko.

  Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelice Mafumiko (kushoto), akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa wahariri, Dar es Salaam.

Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya wahariri wakiwa katika mafunzo hayo.

Baadhi ya maofisa wa ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali wakiwa katika mafunzo hayo

Picha ya pamoja  mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.

…………………………………………………..

Matokeo ya tafiti za magonjwa ya ukanda wa joto yaliyofanywa na maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni Pamoja na ugunduzi wa mbinu za kutambua vijidudu vya ugonjwa wa Malaria iitwayo “Giemsa Stain” ambayo inatumika mpaka sasa.

Hayo yamesemwa na  Mkurugenzi – Idara ya Huduma za Ubora wa Bidhaa kutoka katika Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw.Sabanitho L. Mtega wakati akiwakilisha Mada isemayo “MAJUKUMU YA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI” katika Mafunzo kwa Wahariri na Wanahabari kwenye ofisi za Bohari ya Dawa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mafunzo hayo Bw.Mtega amesema kuwa nje ya ugunduzi vijidudu vya uginjwa wa Malaria pia katika matokeo mengine ambayo wamewahi kuyapata ni pamoja na Ugunduzi wa vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na kuwafanya kufanikiwa kupata tiba ya ugonjwa huo.

Aidha Bw.Mtega amesema kuwa Majukumu ya Mamlaka yamegawanyika katika maeneo mbalimbali kama Kufanya Uchunguzi wa Kimaabara wa Vielelezo/Sampuli mbalimbali,Kusimamia Utekelezaji wa Sheria Tatu (ICCA, HDNA, GCLA Act),Kufanya utafiti kwenye maeneo yanayohusiana na majukumu ya Mamlaka,Utekelezaji wa Programu za kitaifa na kimataifa ikiwemo Mikataba ya Kimataifa inayohusu usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani.

Amesema dhima ya Mamlaka hiyo ni Kutoa Huduma Bora za Kimaabara kwa gharama nafuu, kutoa Ushauri na Utafiti wa Kisayansi-Kemia kwa Serikali, Taasisi na Watu Binafsi (Umma) kwa lengo la kulinda Afya za Wananchi na Mazingira.

Pamoja na hayo amesema moja ya mafanikio kwa Maabara hiyo ni pamoja na Kuwa Maabara Bora inayotambulika na kuaminiwa Kitaifa na Kimataifa katika kushughulikia na kusimamia masuala yote yanayohusu Uchunguzi, Afya, Ustawi wa Jamii na Mazingira.