Home Michezo MWENYEKITI SIMBA AACHIA NGAZI

MWENYEKITI SIMBA AACHIA NGAZI

0

***********************

Mwenyekiti wa Klabu wa Simba Swedi Nkwabi amejiuzulu nafasi hiyo kwa kile alichokieleza kuwa ni kuhitaji muda zaidi wa kusimamia shughuli zake binafsi.

Taarifa iliyotolewa leo na uongozi wa klabu hiyo imeeleza kuwa Swedi amefanya uamuzi huo kwa hiari yake na tayari ameiandikia barua bodi ya wakurugenzi kupitia mwenyekiti wake Mohamed Dewji kuitaarifu juu ya uamuzi wake.

Uongozi wa Simba, kupitia bodi hiyo pamoja na sekretarieti umebariki uamuzi huo na kumtakia kila la heri katika shughuli zake binafsi huku ukimuomba aendelee kushiriki katika shughuli mbalimbali za klabu.

Taarifa hiyo rasmi ya Simba imesema utaratibu wa kumpata mwenyekiti mpya atakayejaza nafasi hiyo utatangazwa baadaye,