Wanaume Mkoani kagera wametakiwa kuwajibika ipasavyo katika kuhakikisha wanaandaa vitu muhimu vitavyosaidia watoto kuepukana na tatizo la utapiamlo kwa watoto wadogo.
Wito huo umetolewa na Mratibu Wa Mradi Wa Mtoto mwerevu Unaojishughulisha na masuala ya lishe kwa kushirikiana na Shirika la Ima World Healith Mkoa kagera.
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake, Mratibu Sista Margaret Ishengoma amesema kuwa tatizo la utapiamlo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano limeendelea kuwaathiri watoto Mkoani humo.
Sista Margaret ameeleza kuwa kutokana na hali hiyo wazazi hususani wanaume wanapaswa kufanya iwezekanavyo kuboresha mahitaji ya msingi ikiwemo ya kuwasaisia akina mama katika malezi ya watoto na kipindi chote cha ujauzito nia na madhumuni ni watoto wahudumiwe kwa kina.
Hatahivyo amefafanua kuwa kundi la wanaume limekuwa halina mwamko katika kupambana na tatizo la udumavu baadala yake huwachia mzigo wa majukumu yote ya Kifamilia akina mama pekee hali inayopelekea wa mama hao kulemewa na majukumu nakusababisha kushindwa kuwahudumia inavyotakiwa watoto hasahasa nyakati za kipindi cha ujauzito.
Vilevile sists huyo ameelekeza kwamba ili mtoto asiathirike na utapiamlo inatakiwa kumuhudumia kwa ukaribu ndani ya siku 1000 tangu kipindi cha ujauzito Wa mama na kabla ya kutimiza miaka miwili ambapo amezitaja baadhi ya athari za udumavu ikiwemo ya kudumaa akili na kusababisha kushindwa kuwa na uwezo Wa kufikiri vizuri kiakili.
Sista Marigaret amevitaja baadhi ya vyakula vya mchanganyiko vinavyotakiwa kutumiwa kama vile Mayai, Maziwa, Samaki, Dagaa karanga, mboga za majani mafuta na vinginevyo na kusisitiza kuwa licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali pamoja na wadau mbambali kuutokomeza udumavu bado tatizo ni kubwa.
Alikadhalika amezitaja takwimu zinavyoonyesha kwa sasa kwa upande wa Kagera ni 38.9% kiwango ambacho bado kinaashiria matokeo mabaya hivyo kila mmoja anapaswa kuchukuwa hatua madhubuti juu kushiriki kupiga vita tatizo hilo katika jamii.