Mkurugenzi mtendaji wa Asasi za Kiraia Bw.Frances Kiwanga akiongea na wadau mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa Ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia inayotarajia kuanza rasmi Novemba 4 hadi 8 mwaka huu jijini Dodoma pamoja na uzinduzi wa tovuti ya Asasi za Kirai.
Wadau mbalimbali wa Asasi za Kirai wakipata picha ya pamoja na Mkurugenzi wa uratibu wa Asasi za kiraia ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Andrew Komba katika uzinduzi wa Ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia inayotarajia kuanza rasmi Novemba 4 hadi 8 mwaka huu jijini Dodoma pamoja na uzinduzi wa tovuti ya Asasi za Kirai.
Mkurugenzi wa uratibu wa Asasi za kiraia ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Andrew Komba akiongea na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa Ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia inayotarajia kuanza rasmi Novemba 4 hadi 8 mwaka huu jijini Dodoma pamoja na uzinduzi wa tovuti ya Asasi za Kirai.
**********************
NA EMMANUEL MBATILO
Ushirikiano kati ya Asasi za Kiraia,Serikali pamoja na wadau wengine wa kimaendeleo ni muhimu kwani ni moja ya njia ambayo itazisaidia asasi hizo kukua kimaendeleo binafsi pamoja na Serikali kiujumla hivyo wataendelea kushirikiana katika kila sekta ili kuzitatua kero na matatizo mbalimbali ya wananchi.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi mtendaji wa Asasi za Kiraia Bw.Frances Kiwanga katika uzinduzi wa Ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia inayotarajia kuanza rasmi Novemba 4 hadi 8 mwaka huu jijini Dodoma pamoja na uzinduzi wa tovuti ya Asasi za Kirai.
Akiongea kwenye uzinduzi huo Bw.Kiwanga amesema wanatarajia kuwa na wiki ya asasi za kirai ambayo itafanyika Novemba 4 mkoani Dodoma yenye lengo la kuiweka asasi hiyo karibu na serikali pamoja na wananchi.
Bw.Kiwanga amesema wao wanajukumu la kuisaidia jamii na kutembea pamoja na serikali katika kuiunga mkono kwenye shughuli za kimaendeleo hususani katika swala la uwajibikaji.
Wakati huo huo Kiwanga amesema wako kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwa kuona kazi nzuri inayofanywa na serikali kupitia michango ya asasi za kiraia pamoja na serikali ya Dkt Magufuli
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uratibu wa Asasi za kiraia ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Andrew Komba amesema wao wanasimamia Asasi nchini kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa kuisaidia Serikali katika kutoa huduma kwa wananchi.
Hata hivyo wiki ya Asasi za Kirai 2019 inatarajiwa kufanyika jijini Dodoma kutoka na ombi lililotolewa na spika wa bunge Mh.Job Ndugai mwaka jana katika maadhimisho ya Asasi za Kiraia yaliyofanyika jijini humo.