Home Mchanganyiko SERIKALI YA TANZANIA IPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI KULETA MAENDELEO

SERIKALI YA TANZANIA IPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI KULETA MAENDELEO

0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
SERIKALI ya Tanzania kupitia sekta binafsi ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hapa nchini.

 

 

 

Ameyasema hayo mwakilishi wa waziri wa viwanda na biashara, waziri wa mambo ya nje, Ramadhan Mwinyi alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa nchini Misri na watanzania wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonesho ya kibiashara yanayofanyika katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.

 

 

“Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hapa nchini katika sekta ya marighafi za ujenzi, nishati ya jua, kemikali pamoja na viwanda vya uhandisi”.

 

 

Nae Rais wa chemba ya wafanyabiashara hapa nchini, Paul Koyi amesema kuwa jukumu lao ni kufanya jambo la kibiashara lisilowezekana kuwezekana ili biashara ziweze kufanyika bila vikwazo. Pia amesema kuwa katika kufanya biashara kunahitaji matendo zaidi na si maneno.

 

 

Amesema hii ni fursa kwa watanzania kuungana na kufanya biashara na wamisri kwaajili ya maendeleo ya nchi pamoja na maendeleo yao wenyewe.

 

 

Wiki ya maonesho ya biashara ya wamisri yanaendelea kufanyika katika hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) jijini Dar es Salaam kuanzia leo Septemba 11 hadi 14, 2019.

 

 

 Waziri wa Mambo ya nje, Ramadhan Mwinyi akizungumza kwa niaba ya waziri wa viwanda na biashara leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya biashara ya wamisri hapa nchini inayoendelea kufanyika katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.

 

 Mkuu wa taasisi ya sekta binafsi (Tpsf), Zachy Mbenna akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya biashara ya Misri na Tanzania inayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14, 2019. Amesema kuwa wafanyabiashara wachukue Fursa hiyo ambapo wafanyabiashara wa nchini Misri wamekuja nchini kuonesha biashara zao katika mambo ya Dawa, marighafi za ujenzi, nishati ya jua, kemikali pamoja na viwanda vya uhandisi ni fursa wa watanzania hapa nchini kujifunza.
 Rais wa  chemba ya biashara, viwanda na kilimo, Paul  koyi akizungumza na wadau wa biashara wa tanzania na wamisri katika uzinduzi wa wiki ya maonesho ya kibiashara ya wafanyabiashara wa Misri yanayoendelea kufanyika katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Misri Nchini Tanzania, Mohamed Abdulwafa akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya maonesho ya kibiashara ya nchi ya Misri hapa nchini yanayoendelea kufanyika katika hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) jijini Dar es Salaam 11 hadi 14 Septemba,2019.
 Waziri wa Mambo ya nje, Ramadhan Mwinyi, Rais wa  chemba ya biashara, viwanda na kilimo, Paul  koyi, Mkuu wa taasisi ya sekta binafsi (Tpsf), Zachy Mbenna na Balozi wa Misri Nchini Tanzania, Mohamed Abdulwafa wakikata utepe kuzinduz wa wiki ya biashara ya wamisri hapa nchini inayoendelea kufanyika katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya nje, Ramadhan Mwinyi, akipata maelekezo kutoka kwa wafanyabiashara wa nchini Misri waliopo katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya nje, Ramadhan Mwinyi, akiangalia vioo vilivyotengenezwa kwa Polycarbonate sheets na wafanyabiashara kutoka Misri yanayoendelea kufanyika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.
 Wadau wa viwanda wakitembelea mabanda ya wamisri katika  hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja.