************************
Mwandishi wa habari za Kiuchunguzi Sebastian Emmanuel Atilio ameshindwa kupata dhamana Leo tangu alipokamatwa tarehe 07/09/2019 na kituo cha polisi Mafinga.
Kwamba wakili wake Emmanuel Chengula alifile maombi mahakama kuu kuomba apelekwe mahakaman au apewe dhamana na polisi wajieleze kwanini sana mshikiria bila utaratibu.
Leo majira ya saa sita mchana walimfikisha katika mahakama ya wilaya mufindi mafinga akikabiliwa kwa makosa mawili katika kesi ya jinai namba 208 ya 2019;
Mosi kutoa taarifa za uongo pili kufanya kazi ya uandishi wa habari bila kutambuliwa na bodi.
Pamoja na hayo upande wa mashtaka umefile maombi namba 11 ya 2019 ya kuzuia dhamana kwa kigezo kwamba usalama wake upo hatarini kwani wananchi wa kijiji cha ifupila wana hasira nae.
Ifahamike kwamba Sebastian Emmanuel Atilio anatuhumiwa kutuma ujumbe tarehe 06/09/2019 kwamba kijiji cha ifupila kipo mbioni kufutwa kwa sharia za ardhi kwani kampuni ya chai ya Unilever Tea Tanzania imeweka mipaka yake(beacons) ndani ya kijiji.