Home Mchanganyiko Abdallah Hussein aing’arisha Dar kwenye mchezo Pool.

Abdallah Hussein aing’arisha Dar kwenye mchezo Pool.

0

Mchezaji wa Pool, Abdallah Hussein(Dar) akicheza dhidi ya
mpinzani wake Baraka Jackson(Manyara) katika mchezo wa
kirafiki uliobeba dhima ya mikoa uliochezwa mwishoni mwa
wiki katika Ukumbi wa Soccer City jijini Dar es Salaam.Abdallah
Hussein alishinda na kuzawadiwa pesa taslimu shilingi milioni
moja (1,000 000/=) kwa udhamini wa Kenice, GJL Commodity
Investment Limited na Ashishi Cinematographer Studio

Mwakilishi kutoka Sportpesa, Levis Paul(kulia) akimkabidhi
Abdallah Hussein(Dar) pesa taslimu shilingi milioni moja (1,000
000/=) marabaada baada ya kuibuka mshindi dhidi ya Baraka
Jackson(Manyara) katika mchezo wa kirafiki uliochezwa
mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Soccer City Sinza jijini
Dar es Salaam uliobeba dhima ya mikoa kwa udhamini wa
Kenice, GJL Commodity Investment Limited na Ashishi
Cinematographer Studio.

***********************

MCHEZAJI wa wa mchezo wa Pool,Abdalah Hussein
mkazi wa jijini Dar es Salaam,Mkoa wa Kimichezo wa
Kinondoni Klabu ya Topland Magomeni ameibuka bingwa
kwa ushoindi wa 8-6 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya
Baraka Jackson kutoka Manyara katika mchezo wa
kirafiki uliochezwa mwishoni mwa wiki uliofanyika katika
Ukumbi wa Soccer City Sinza jijini Dar es Salam uliobeba
dhima za Mikoa yao yaani Dar es Salaam dhidi ya
Manyara na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi
milioni moja(1,000 000/=) uliodhaminiwa na Kampuni ya
Kenice, GJL Commodity Investment Limited na Ashishi
Cinematographer Studio .

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa
Chama cha Pool Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni
kwanza aliwashukukuru wachezani kwa ushindani
waliounyesha mbele ya wadau wapenda mchezo huo
waliojitokeza kushuhudua, lakini pia alilmpongeza bingwa
Abdaah Husseini kwa ushindi na kumuomba pesa
aliyoipata akaitumie vizuri kuweka kumbukumbu katika
maisha yake ya ushindi wake.
Nae Bingwa Abdallah Hussein alimshukuru waandaaji wa
mchezo huo na kuwaomba wasikate tamaa na
changamoto za hapa na pale wanazokutana nazo kwani
wao kama wachezaji wako pamoja na wao katika
kuhakikisha mchezo unafika tunakohitaji.

Lakini pia Abdallah alishukuru kwa zawadi aliyoipata
kwani ataitumia kwa matumizi sahihi kama historia ya
ushindi huo.
Nae Baraka Jacksoni kutoka Manyara aliwashukuru
waandaaji na kumpongeza Abdallah Hussein kwa ushindi
lakini alikiri uzoefu ndio sababu kubwa ya kushindwa
lakini anaamini siku nyingine akipata nafasi ya kucheza
nae atashinda.
Mchezo huo ulihudhuriwa na mamia ya
wanamichezo,wapenzi na wadau wa mchezo wa Pool
ambao walidhihisha kweli mchezo huo unapendwa sana
nchini Tanzania.