Home Mchanganyiko WAZIRI JAPHET HASUNGA AMALIZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU SITA NCHINI ISRAEL,...

WAZIRI JAPHET HASUNGA AMALIZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU SITA NCHINI ISRAEL, ASEMA UTAFITI WA KILIMO NA TEKNOLOJIA ZA ISRAEL UTAINUFAISHA TANZANIA

0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiagana na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion Jijini Tel Aviv, nchini Israel baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya siku sita. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) jana alfajiri tarehe 8 Septemba 2019 amerejea nchini baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya siku sita nchini Israel iliyoanza tarehe 1 Septemba
2019 na kumalizika tarehe 7 Septemba 2019.
 
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion Jijini
Tel Aviv, Mhe Hasunga ameagwa na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima.
Katika ziara hiyo Mhe Hasunga alishiriki mahafali
ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yaliyofanyika Jijini Jerusalem, Mahafali hayo yalijumuisha vijana 1600 kutoka mataifa zaidi ya 12 ambapo kati ya hao vijana 45 ni watanzania, Pia alitoa vyeti kwa vijana hao wa Tanzania 45 waliohitimu.

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi Cheti Dayana Novat wakati wa mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ICC (Jerusalem International Conventional Center) Jijini Jerusalem nchini Israel, Tarehe 2 Septemba 2019.


Akizungumza na vijana hao 45 mara baada ya mahafali
ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies, Mhe
Hasunga aliwahakikishia kuwa Serikali imeridhia ombi lao la kuwapatia ardhi kwa
ajili ya kuwekeza kwenye sekta ya Kilimo.
Alisema
kuwa serikali ya Tanzania ina ardhi nzuri yenye rutuba ambayo haijaguswa kwa
ajili ya kilimo hivyo huo ni muda mwafaka kwa vijana hao kupatiwa ardhi kwa
ajili ya kuonyesha kwa vitendo waliyofundishwa wakati wa masomo yao nchini
Israel.
Mhe Hasunga alisema
kuwa ni wakati muafaka kwa wanafunzi hao kutumia ujuzi walioupata wa kujifunza
mbinu bora na teknolojia za kisasa za kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ili
kutoa elimu ya kilimo hicho nchini mwao pindi watakaporejea.
Amesema kuwa nafasi
hizo za masomo ya kilimo nchini Israel zimetoa fursa kwa wataalamu hao kuongeza
ufanisi katika Sekta ya kilimo hivyo watakaporejea nchini wanapaswa
kukibadilisha kilimo kuwa na tija zaidi katika uzalishaji.
Aidha, alisema
kuwa, tatizo kubwa la Sekta ya Kilimo nchini ni uzalishaji mdogo usiokuwa na
tija ambapo wakulima hutumia nguvu kubwa lakini matokeo yanakuwa madogo. hivyo,
alisisitiza kuwa, watakaporejea nchini Tanzania wanatakiwa kutoa elimu kwa
wakulima ya kuzingatia mbinu bora za kilimo, matumizi sahihi ya pembejeo,
mbolea na pia kutumia mbegu bora ili kuweza kumnufaisha mkulima.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana waliohitimu mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yaliyofanyika jijini Jerusalem nchini Israel, tarehe 2 Septemba 2019.

Katika ziara hiyo nchini Israel Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen na kuridhia kwa kauli moja kuwa serikali za nchi hizo mbili kuingia makubaliano ya kuendeleza kilimo hususani katika utafiti, Tija katika uzalishaji, na Teknolojia.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima, Mhe Hasunga ametoa shukrani kwa Serikali ya Israeli kuipatia Tanzania nafasi 100 za kujifunza kuhusu sekta ya kilimo kwa vijana kupitia programu inayosimamiwa na Agrostudies.
Waziri Hasunga alieleza katika mkutano huo dhamira ya Serikali ya Tanzania inayoongoza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli, ya kuwasaidia
vijana waliorudi nyumbani baada ya mafunzo hayo kwa kuanza kuwapatia mahitaji ya msingi ikiwemo ardhi ambayo ipo eneo litakalowawezesha kujiendeleza.

Sambamba na hayo Waziri Hasunga alizungumzia kuhusu maeneo yanayoweza kuwavutia wawekezaji kutoka Israeli ili kuwekeza nchini Tanzania kwa kutoa takwimu za ukubwa wa ardhi yenye rutuba, uwepo wa maji na hali ya hewa inayoruhusu ukuaji wa aina
nyingi za mazao.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Israeli Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa nchi hiyo Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen alimuhakikishia Waziri Hasunga kuwa Serikali ya Israeli ipo tayari kusaini hati ya makubaliano ya kilimo (Memorandum Of Undarstanding-MOU) hivyo Serikali ya Tanzania itatakiwa kuwasilisha haraka mahitaji hasa kwenye mazao ambayo muhimu ya kuanza nayo kwa ajili ya soko la Israel.

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.

Pia, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) alikutana na kufanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari katika kikao kilichofanyika kwenye Ofisi za kampuni hiyo zilizopo Jijini Tel Aviv.
Mhe Hasunga alimualika Bi Sivan kutembelea nchini Tanzania ili kuwekeza kadhalika kusaidia katika maeneo mbalimbal. Alisema kuwa kampuni hiyo inatakiwa kuongeza mshikamano na serikali ya
Tanzania ili kuendelea kutatua sehemu ya matatizo ya wananchi sambamba na kuimarisha mp
ango wao wa kutoa suluhisho la Israeli na ujuzi kwa wale wanaohitaji kuishi katika vijiji vya Kiafrika.
Waziri Hasunga amemuhakikishia Bi Ya’ari kuwa Tanzania ni nchi nzuri katika uwekezaji na sehemu salama ya kuishi huku serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ikiendeleza juhudi za kuboresha maisha ya watanzania na kuimarisha uchumi wa nchi.
Hata hivyo ameipongeza kampuni hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika nchi za Afrika katika sekta ya nishati ya jua ikiwa ni pamoja na mchango wao katika kutekeleza miradi ya maji safi, na Kusaidia vituo vya watoto yatima.
Alisema kuwa Tanzania ni sehemu salama na imara katika uwekezaji, kwani serikali imeanzisha kituo cha uwekezaji (TIC)
ambacho ni Taasisi ya msingi ya serikali yenye jukumu la kuratibu, kuhimiza, kukuza na kuwezesha uwekezaji.
Kwa upande wake Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari akizungumza katika kikao kazi hicho aliridhia ombi la Waziri Hasunga la kuongeza uwezekano wa kuisaidia Tanzania na kusema kuwa mwanzoni mwa mwezi wa tisa atawasili nchini Tanzania kwa ajili ya kuainisha
maeneo ya uwekezaji.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo tarehe 4 Septemba 2019 Jijini Tel Aviv nchini Israel akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 6. Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima.

Vilevile Mhe Hasunga alitembelea shamba la utafiti wa kilimo na kukutana na Mkuu wa Mradi wa Umwagiji Afrika wa kampuni ya Netafim Ndg Shay Haxter ambapo alimualika kutembelea nchini Tanzania kwa ajili ya uwekezaji kwenye sekta ya kilimo.

Mhe Hasunga alisema kuwa Tanzania kuna maeneo makubwa yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ikiwemo eneo la Rufiji ambako ujenzi wa mradi wa umeme wa Bwawa la Nyerere unaendelea na punde utakapokamilika kuna matarajio ya kuwa na wastani wa hekta 150,000 zinazofaa kwa kilimo.
Waziri Hasunga pia alikutana na kuzungumza na baadhi ya wanafunzi wa Tanzania walioshiriki mafunzo ya Kilimo nchini Israel kwenye shamba la mifugo la Jacob’s Farm na kujionea jinsi walivyonufaika na mafunzo hayo.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kulia) akizungumza na Mkuu wa Mradi wa Umwagiji Afrika kampuni ya Netafim Ndg Shay Haxter mara baada ya kutembelea katika shamba la utafiti wa kilimo wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku sita nchini Israel. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na baadhi
ya wanafunzi wa Tanzania walioshiriki mafunzo ya Kilimo nchini Israel kwenye shamba la mifugo la Jacob’s Farm, Mwingine pichani ni
Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima (Kulia),tarehe 3 Septemba 2019.
 
Katika ziara hiyo ya kikazi Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga alikutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Wakurugenzi 6 wa Taasisi ya Mashav wa Wizara ya Mambo ya nje
ya Israel. Ambapo mkutano huo ulihudhuriwa pia
na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya agrostudies Ndg Yaron Tamir.
Katika mkutano huo wa kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem Waziri Hasunga aliishukuru serikali ya Israel kwa kukubali ombi la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli la kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoshiriki mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies katika kipindi cha mwaka mmoja kutoka 45 ambapo imefikia idadi ya wanafunzi
100.
Kadhalika kikao hicho kilijadili kwa kina namna ya kuboresha zaidi mahusiano baina ya nchi ya Tanzania na Israel hususani katika kuimarisha ushirikiano kwenye nyanja za utafiti, uongezaji
thamani wa mazao, na namna ya kuongeza ukubwa wa mashamba ya kilimo na tija.