Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA uliofanyika leo kwenye jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA uliofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Ubungo Plaza huku Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt. Agnes Kijazi wa pili kutoka kushoto na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi sekta ya Uchukuzi Bw. Leonald Chamriho kushoto na viongozi wengine wakipiga makofi.
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akionesha cheti hicho mara baada ya uzinduzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA uliofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Ubungo Plaza huku Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt. Agnes Kijazi wa pili kutoka kushoto na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi sekta ya Uchukuzi Bw. Leonald Chamriho.
………………………………………………
Serikali imesema itaendelea kuboresha Huduma za Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ambapo kwa sasa imekamilisha manunuzi ya rada tatu kwa kutoa fedha ili kuwa na rada saba zilizoahidiwa ambazo zitakidhi matakwa ya nchi nzima na kuwapatia eneo Dodoma kwa ajili ya kujenga Makao Makuu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe leo Septemba 5,2019 wakati akizindua
rasmi Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuwa Mamlaka kisheria kutoka kuwa Wakala.
Waziri Kamwelwe ameongeza kuwa, lengo la serikali ni kuwa na rada saba za hali ya hewa na tayari zipo mbili Dar es Salaam na mwanza huku tayari wameanza kutoa fedha kwa ununuzi wa rada tatu zitakazofungwa Mtwara,Kigoma na Mbeya ambazo zitaiwezesha mamlaka hiyo kufanya kazi kwa ufanisi
Aidha Waziri amewaahidi wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuwaangalia kwa jicho jingine katika kuwawezesha kuongezwa mishahara kwani licha ya kiwango kidogo wamefanya kazi kwa ufanisi wakati shughuli zao haziwawezeshi kufanya miradi mingine.
Amesema serikali itaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili kuweza kufanikisha lengo la kufikia uchumi wa kati katika mwaka 2025 na kuyafikia malengo ya kitaifa ya maendeleo endelevu na kuakisi dira ya taiafa ya maendeleo ya mwaka 2025 na mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dkt. Agnes Kijazi amesema Mamlaka ya Hali ya Hewa Duniani (WMO) katika utaratibu wake linatambua mchango wa vituo vya hali ya hewa vya muda mrefu katika utoaji huduma hiyo ambapo mwaka huu wametambua vituo viwili nchini vya Bukoba na Songea kwa kutoa taarifa za hali ya hewa kwa usahihi kwa miaka zaidi ya 100.
Hii imetokana na umuhimu wa shughuli za hali ya hewa nchini na kuifanya kuwa mamlaka kamili,” amesema Dkt Kijazi
Pia Dkt. Kijazi amekabidhi vyeti viwili kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambayo imevitambua vituo viwili vya kusoma utabiri vya Songea na Bukoba.