***********
Na Queen Lema, Arusha
zaidi ya mawakili 2000 kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini wanatarajiwa kupatiwa elimu juu masuala mbalimbali yahusuyo kazi zao na jamii kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha kazi zao kwenye umma unaowazunguka
aidha mawakili hao wanatokea maeneo mbalimbali na watapewa elimu hiyo kwa kushirikiana na wanadau mbalimbali ambao wanawasilisha mada kwenye semina inayoendelea jijini arusha
akizungumza na fuulshangwe mapema leo afisa programu msaidizi kitengo cha mafunzo endelevu kwa mawakili kutoka chama cha mawakili (TLS)bi Rose Salvatory alisema mawakili hao watajifunza na kupatiwa mafunzo kwenye mada za muhimu ambazo ni nane
bi rose alifafanua kupitia mada hizo ambazo zitatolewa zitaweza kuwajengea uwezo wa namna ya kuendeleza taaluma yao lakini hata kuisaida serikali hususani kwa nyakati kama hizi za uchumi wa viwanda
‘kwa mfani unapoangalia katika mada hizi tuna mada juu ya makampuni ya biashara tunaaamini kuwa mtu kama wakili akiwa na anajua sheria hii ana uwezowa kumsaidia mtu mpaka kufikia hatua ya mwishi na baadae nchi ikapata mapato kwa hiyo ndio vitu vya msingi ambavyo tunaviangalia”aliongeza
Amefafanua kuwa elimu juu ya mada hizo ambazo zitakuwa na mwangaza mkubwa kwa mawakili lakini pia zitaweza kuwaongeze pointi 2 kati ya 10 ambazo wanatakiwa kuwa nazo kila mwaka kwa mujibu wa sheria ya chama hicho
“kila mwaka wakili lazima apate jumla ya pointi 10 na akama akikikosa huwa kuna sababau sasa kupitia mafunzo haya hawa mawakili wataweza kujivunia pointi zao 2 nawasihi hata wale ambao hawajapata mafunzo haya waje ili wafikie malengo na waisaidae jamii kwa elimu watakayopata”aliongeza
katika hatua nyingine baadhi ya washiriki waliopata mafunzo kwenye semina hiyo walisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa kuwa mbali na kupata alama 2 kati ya 10 lakini pia yanawasaidia kupata mbinu mbalimbali za kuikomboa jamii