Home Mchanganyiko JESHI LA POLISI KIKOSI CHA RELI CHATOA ELIMU KWA ABIRIA WANAOTUMIA...

JESHI LA POLISI KIKOSI CHA RELI CHATOA ELIMU KWA ABIRIA WANAOTUMIA USAFIRI HUO.

0

***************

Jeshi la Polisi kupitia kikosi chake cha Reli leo kimetoa Elimu kwa Abiria
wanaotumia usafiri wa Treni juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na uhalifu
unaofanywa na baadhi wa matapeli, elimu hiyo imetolewa na SGT Michael,
eneo la kamata kariakoo jijini Dar Es Salaam mapema leo kabla abiria hao
kuanza safari ya kuelekea Mkoani Kigoma. Huku akisema kwa kipindi kifupi
ambacho safiri za treni zilisimama baadhi ya watu walitumia nafasi hiyo kama
sehemu ya kujipatia kipato kwa kuwatapeli abiria kwa njia ya kukatisha tiketi
feki.

Aidha katika hatua nyingine SGT Michael aliwataka wanandoa pamoja na
watu wengine wanaotumia usafiri huo kuacha kuwafanyia ukatili wa kijinsia
wenza wao au watoto wao huku akisema kuna baadhi watu husafirisha familia
zao hasa kwa wanawake wajawazito ambao wamekaribia kujifungua hali hiyo
huwapelekea wanawake hao kujifungulia ndani ya Treni.